Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji ,akikagua mabanda ya wamiliki wa Alama za Bidhaa wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya udhibiti bidhaa bandia Duniani leo Juni 13,2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji ,akikagua mabanda ya wamiliki wa Alama za Bidhaa wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya udhibiti bidhaa bandia Duniani leo Juni 13,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti kamati ya Kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe.David Kihenzile ,akitoa salamu za Kamati yake wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya udhibiti bidhaa bandia Duniani leo Juni 13,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ushindani (FCC) Dkt.Aggrey Mlimuka ,akizungumza wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya udhibiti bidhaa bandia Duniani leo Juni 13,2023 jijini Dodoma.
MKurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) Bw.William Erio,akizungumza wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya udhibiti bidhaa bandia Duniani leo Juni 13,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani halali ya biashara Zanzibar Mohammed Sijari Mohammed,akitoa salamu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya udhibiti bidhaa bandia Duniani leo Juni 13,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la maadhimisho ya siku ya udhibiti bidhaa bandia Duniani leo Juni 13,2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji ,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kongamano la maadhimisho ya siku ya udhibiti bidhaa bandia Duniani leo Juni 13,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA.
SERIKALI imesema katika kipindi cha miezi tisa ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/2023, kiwango cha bidhaa bandia zinazoingia nchini zinaendelea kushuka ambapo Tume ya ushindani (FCC) ilikagua makasha ya kusafirishia mizigo 7918 katika Bandari ya Dar es Salaam, kati ya hayo makasha 206 tu, sawa na asilimia 2.6, yalikutwa yakiwa na shehena ya bidhaa zinazokiuka Sheria ya Alama za Bidhaa.
Hayo yamesema leo Juni 13,2023 jijini Dodoma na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji wakati akifungua kongamano la maadhimisho ya siku ya udhibiti bidhaa bandia Duniani.
Dkt.Kijaji amesema hali hiyo inamaanisha kuwa asilimia 97.4 ya bidhaa zote zilizokaguliwa katika kipindi hicho, zilikidhi matakwa ya Sheria ya Alama za Bidhaa na hivyo kuwa bidhaa halali.
“Takwimu hizi zinaonesha wazi kuwa FCC kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali na waagizaji na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali wanafanya kazi nzuri na kuifanya nchi yetu kuwa ni sehemu nzuri ya kuwekeza kwa nia ya kuzalisha bidhaa mbalimbali, sehemu nzuri ya kufanya biashara na kujenga viwanda,”amesema Dkt.Kijaji
Aidha Waziri Kijaji amesema ni muhimu kuhakikisha hizo asilimia 2.6 ya bidhaa bandia zinazoingia nchini ni ishara ya mafanikio na kwamba kukitokea uzembe kidogo basi asilimia hizo zinaweza kuongezeka kwa kasi.
Hata hivyo Dkt.Kijaji ametoa wito kwa Tume hiyo ya Ushindani na wadau wengine kuongeza ushirikiano katika kutoa elimu kwa wadau kuhusu madhara ya bidhaa bandia na jinsi ya kuzitambua na kuendelea kukaa na waagizaji wakubwa wa bidhaa kutoaingiza nchini bidhaa bandia.
“Niwatake Wakala wa Ushuru wa Forodha kutokukubali kusafirisha na kuingiza bidhaa bandia lakini pia Balozi za nchi ambazo bidhaa zake zinapita katika nchi ya Tanzania kwa kushirikiana na mamlaka husika katika nchi zao wanapaswa kuwaelimisha wafanyabiashara wao kutokuagiza na kupitisha bidhaa bandia nchini Tanzania,”amesisitiza
Kwa upande wa Mashirika ya Kimataifa na Asasi mbalimbali za uwezeshaji wa kibiashara Waziri Kijaji ameitaka FCC kuzisaidia katika kupata mafunzo na nyenzo za kisasa za kutambua na kudhibiti bidhaa bandia ikiwa ni pamoja na kuuelimisha umma kuhusu madhara ya bidhaa bandia na hivyo kuwashauri waepuke kuzinunua.
Dkt.Kijaji amesema Wizara hiyo itasimamia ukamilishaji wa maboresho ya Sheria ya Alama za Bidhaa katika kuunga mkono juhudi hizo na kuleta ufanisi zaidi kiutendaji.
“Natambua kuwa FCC kwa muda mrefu ilikuwa imejikita zaidi katika kaguzi kwenye bandari ya Dar es Salaam pamoja na bandari zake kavu zipatazo 15,eneo la ukaguzi kwa sasa linaongezeka ambapo kutakuwa na Bandari Kavu ya Kwala, Mkoani Pwani, pamoja na vituo vya ukaguzi wa pamoja mipakani vilivyojengwa na vinavyoendelea kujengwa kwa uratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,”amefafanua.
Kwa mujibu wa ratiba ya kongamano hilo mada mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa huku kukiwa na matarajio ya mapendekezo ya namna bora ya kuboresha uhusiano kati ya sekta ya umma na binafsi katika kupambana na bidhaa bandia katika maeneo yatakayoonekana yanahitaji juhudi za pamoja.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya FCC Dkt.Aggrey Mlimuka amesema FCC inaongoza shughuli za kikosi kazi katika kuondokana na bidhaa bandia na kulifanya soko la bidhaa kuwa la uhakika na kuaminika kwa wafanyabiasha.
Dkt.Mlimuka amesema kuwa tumekuwa tukifanya kaguzi mbalimnali ikiwemo bandari ya Dar Es Salaam na bandari zake kavu zipatazo 15 ikiwa ni pamoja na kufungua ofisi za kanda katika mikoa ya mwanza ,Mbeya na arusha ambazo hurahisisha kaguzi kwenye masoko ,mipaka na vituo vingine vya ukaguzi.
”Tunafanya kaguzi za kushtukiza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na kukamata bidhaa bandia natoa wito kwa wadau wa maendeleo kufanya biashara kihalali na kuondokana na usumbufu wa bidhaa bandia.”amesema Dkt.Mlimuka
Pia amesema kuwa FCC imeendeleza ujuzi zaidi wa kutambua na kudhibiti bidhaa bandia ikiwa ni pamoja na kuuelimisha umma kuhusu madhara ya bidhaa hizo na hivyo kuwashauri waepuke kuzinunua.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani halali ya biashara Zanzibar Bw.Mohammed Sijari Mohammed,amesema Taasisi hizi mbili zina mahusiano ya karibu na kusaidia kuimarisha utendaji kazi katika kudhibiti bidhaa zisizo halali.
”Jitihada zinaendelea kwa pande zote mbili za Muungano na kunafanya kazi kwa kusimamia maadili bila kuwaonea watu.”amesema