Mkurugenzi wa Miradi kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Boniface Mkumbo, akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Balozi Eng. Aisha Amour, kuhusu namna usimamizi wa Daraja jipya la Wami unavyofanywa mkoani Pwani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Balozi Eng. Aisha Amour, akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Miradi kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Boniface Mkumbo (aliyevaa kofia), mara baada ya menejimenti ya Sekta hiyo kukagua Daraja jipya la Wami lililokamilika kujengwa mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Tafiti kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Mussa Mataka, akionesha teknolojia mpya waliyoijaribu katika moja ya barabara kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Balozi Eng. Aisha Amour pamoja na menejimenti ya Sekta hiyo, mkoani Tanga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Balozi Eng. Aisha Amour, akitoa maelekezo kwa menejimenti ya Sekta hiyo kuhusu usimamizi wa miradi ya barabara nchini, mkoani Tanga.
Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Alois Matei, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Sekta hiyo Balozi Eng. Aisha Amour, wakati viongozi hao walipokagua usimamizi wa miradi, mkoani Tanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Mussa Kashinde akifafanua jambo kwa menejimenti ya Sekta hiyo (hawapo pichani), wakati walipokuwa katika ukaguzi wa Daraja jipya la Wami, mkoani Pwani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Balozi Eng. Aisha Amour, akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya menejimenti ya Sekta hiyo, mkoani Pwani.