Na Mwandishi Wetu-Tabora
Shirika la Akili Platform Tanzania limeendelea kuunganisha vijana waliopo katika mfumo wa elimu ya vyuo pamoja na wenye ulemavu Mkoa wa Tabora kwa kuwapatia elimu juu ya kilimo mviringo na elimu ya kujitegemea ili kutunza mazingira na kuongeza kiwango cha uchumi kwa mtu mmoja mmoja , familia na Taifa.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Roghat Robert na Afisa mawasiliano, Gift Emmanuel, wakati wa mafunzo kwa vijana kuhusiana na elimu ya kujitegemea mkoani Tabora.
Katika mafunzo hayo vijana wameunganisha kutoka chuo cha Reli Tabora kwa kupata mafunzo juu ya kilimo cha mviringo ambapo jumla ya mifuko zaidi ya180 imelimwa mazao ya muda mfupi ikiongozwa na mbegu za chainizi.
Mwalimu mlezi wa wanafunzi wa chuo cha Reli John Maina amesema ni baraka kwa wanachuo wake pamoja na Walimu pamoja na wafanyakazi wote.
Ameshukuru sana Shirika la Akili Platform Tanzania kwa kuanzisha mfumo wa kuunganisha vijana na wenye ulemavu na fursa za mazingira kupitia kazi za mikona na elimu ya kujitegemea.
Mwenyekiti wa Club ya akili platform Tanzania Filbert Innocent amesema hii ni njia ya kuendelea kutunza mazingira kwani mifuko hii ilikuwa ikichomwa ila sasa kupitia Akili platform Tanzania idara ya mazingira wameona ni fursa kwa vijana na kweli inafungua akili za wengi waliokuwa hawajui nini wafanye.
Naye Katibu Mtendaji wa Club ya Akili platfom Tanzania Astelia Safari, amesema njia hii ya Shirika la Akili Platform Tanzania itasaidia mabinti wengi kwani hushidwa kujitegemea wenyewe ila kupitia hii program ya nisaidie nifanye mwenyewe kupitia kilimo mviringo .
‘Kuna mazao mengi ya kulimwa na kupata faida kwa mtaji mdogo ameomba mabinti wanaelekea kuhitimu chuo wazingatie elimu hii kwani itawakomboa wakati wakisubilia ajira’ amesema.
Naye Kishosha Kulwa kiongozi wa Idara ya Mazingira Chuo cha Reli amesema mwanzo hakujua kama anaweza kuingiza pesa akiwa ni mwanafunzi kupitia kilimo ila sasa anaona fursa nyingi sana na amesema kazi za mikono ni daraja la mafanikio.
Gift Emmanuel Afisa mawasiliano Akili Platform Tanzania amesema huu ni mwendelezo wa shughuli zetu za taasisi.
Roghat F Robert ni Mkurugenzi wa Shirika la Akili Platform Tanzania amehitimisha kwa kushukuru viongozi wa dini, Serikali na waandishi wa habari kwa kuungana na Akili platform Tanzania katika nyakati zote pia ameomba wakuu wa shule , vyuo na wadau wa maendeleo kuendelea kumuunga mkono katika program hii kwani lengo ni kuweka fursa kwa vijana na jamii kwa ujumla.
Amesema ni wazi hotel kubwa zote na ndogo wamelenga kuwahudumia kupitia kilimo cha mviringo.
Ameomba Watanzania wenye mapenzi mema kuzidi kujitoa kuwezesha shughuli kwa taarifa kwa njia ya simu 0626 551 859 Akili Platform Tanzania au [email protected]
Ikiwa unaona familia yenye mtoto mwenye ulemavu wa akili ulipo.