Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akiongea katika mkutano wa jukwaa la maendeleo ya ushirika mkoa wa Arusha lililofanyika katika ukumbi wa club D uliopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akimkabidhi funguo wa gari na gari Mrajis wa vyama vya ushirika mkoa wa Arusha Grace Masambaji kwa ajili ya kutumia kwa shughuli za chama hicho mkoani hapo gari hilo lilitolewa na mdau wa ushirika ambao Shirika la Heirfer.
Julieth Laizer,Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Arusha,John Mongela amewataka viongozi wa vyama vya ushirika mkoani hapa kuacha tabia ya kuanzisha migogoro kwa lengo la kujinufaisha kwa masilahi yao binasfisi hali ambayo inapelekea kuharibu taswira ya vyama hivyo katika jamii.
Akizungumza katika jukwaa la maendeleo ya ushirika mkoa wa Arusha ,Mongela amesema kuwa kumekuwepo na baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika wamekuwa wanaanzisha migogoro makusudi kwa lengo lao la kujipatia maslahi yao binafsi.
“Unakuta kiongozi wa chama anatafuta namna ya kuhujumu ushirika , anafanya jambo la kichama kwa mlengo wake bila kushirikisha wanachama jambo ambalo linaleta migogoro na wanachama hali hii sio taswira nzuri,”amesema Mongela.
Aidha amewataka viongozi wa ushirika wafanye kazi ya kuamasisha wananchi kuunda vyama vya ushirika ili vyama viwe vingi zaidi huku akibainisha kuwa ndani ya vyama hivyo kuna fursa nyingi zaidi ambazo zitawainua kiuchumi.
Mongela amesema ndani ya ushirika taasisi za kibenki zipo tayari kushirikiana nao na kwa wale wakulima serikali imerahisisha ata riba zimeshushwa na kuna fedha nyingi ambayo wapo wengi haijawafikia na itakuwa na tija nyingi na fedha hiyo sio kwa ajili ya kilimo cha shambani tu bali inawahusu hata wale ambao wanaongeza dhamani mazao .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa jukwaa la maendeleo ya ushirika mkoa wa Arusha Wilibald Ngambeki amesema kuwa katika vyama vyao vya ushirika wanakabiliwa na tatizo la Tehama kwa upande wa mijini inarahisisha kazi lakini kwa upande wa vijijini ni kikwazo kwa maendeleo ya ushirika kwani baadhi ya maeneo ya vijijini hayana huduma za intanet na kama ipo ni yaubora wa chini .
Aidha aliomba serikali kupitia mamlaka ya mapato Tanzania kuacha kulazimisha matumizi ya Tehama kwenye ku-file returns kwa walipa kodi wote na badala yake wakubali matumizi ya njia zote ikiwemo ile ya zamani yakupeleka makaratasi hasa kwa vyama vilivyopo vijijini pamoja na kwamba yapo maboresho yanayoendelea kwenye mfumo wa kujaza ritani za kodi bado mfumo huo unachangamoto kwa watumiaji.
Amesema kuwa vyama vya ushirika vilivyo vingi na hasa vya kijamii vinaanza kama kikundi vya kusaidiana inapofika hatua uamuzi ukafanywa wa kuanzisha chama chama ushirika ina hama na ile miamala ya nyuma bahati mbaya vikundi hivi havina uelewa wa maswala ya kodi hivyo kujikuta na adhabu zinazotokana na kushindwa kufuata taratibu za kodi .
Aidha kutokana na hilo waliomba vyama vya ushirika kupewa likizo hadi miaka 10 kabla ya kufuata za kikodi ili kuwezesha chama kujenga uwezo wa ndani ikiwemo uwezo wa kuajiri wataalamu.