NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Deogratius Ndejembi,pamoja na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Godwin Gondwe wakifanya usafi wa mazingira katika mitaa ya barabara ya saba ya nane pamoja ya tisa leo Juni 3,2023 jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya siku ya mazingira duniani yatakayofanyika Juni 5, mwaka huu.
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Deogratius Ndejembi,akipanda mti katika eneo la la Mji mpya leo Juni 3,2023 jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya siku ya mazingira duniani yatakayofanyika Juni 5, mwaka huu.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Godwin Gondwe,akipanda mti katika eneo la la Mji mpya leo Juni 3,2023 jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya siku ya mazingira duniani yatakayofanyika Juni 5, mwaka huu.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama ,akipanda mti katika eneo la la Mji mpya leo Juni 3,2023 jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya siku ya mazingira duniani yatakayofanyika Juni 5, mwaka huu.
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Deogratius Ndejembi,akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wakazi wa jiji la Dodoma (hawapo pichani) leo Juni 3,2023 mara baada ya kufanya usafi wa mazingira katika mitaa ya barabara ya saba ya nane pamoja ya tisa ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya siku ya mazingira duniani yatakayofanyika Juni 5, mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemarry Senyamule ,akizungumza mara baada ya kufanya usafi wa mazingira katika mitaa ya barabara ya saba ya nane pamoja ya tisa ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya siku ya mazingira duniani yatakayofanyika Juni 5, mwaka huu leo Juni 3,2023 jijini Dodoma.
Mkuu wa wilaya ya Bahi Godwin Gondwe ,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya usafi wa mazingira katika mitaa ya barabara ya saba ya nane pamoja ya tisa ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya siku ya mazingira duniani yatakayofanyika Juni 5, mwaka huu leo Juni 3,2023 jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama ,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya usafi wa mazingira katika mitaa ya barabara ya saba ya nane pamoja ya tisa ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya siku ya mazingira duniani yatakayofanyika Juni 5, mwaka huu leo Juni 3,2023 jijini Dodoma.
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Deogratius Ndejembi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya usafi wa mazingira katika mitaa ya barabara ya saba ya nane pamoja ya tisa ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya siku ya mazingira duniani yatakayofanyika Juni 5, mwaka huu leo Juni 3,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
NAIBU waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Deogratius Ndejembi,amewataka viongozi wa mitaa, vitongoji,vijiji pamoja na kata nchini kuhamasisha wananchi kushiriki kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kuendelea kuhifadhi mazingira.
Mhe.Ndejembi, ameyasema hayo leo Juni 3,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wakazi wa jiji la Dodoma mara baada ya kufanya usafi katika eneo la barabara ya saba ya nane pamoja ya tisa na Mji mpya ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimishi ya siku ya mazingira duniani juni 5, mwaka huu.
Ndejembe amesema kuwa Viongozi hao wanatakiwa kuwahamasisha wananchi kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwishi na sio kusubiri hadi siku za maadhimisho kama hayo.
“Niagize pia halmashauri zote nchini kila wanapopima viwanja wahakikishe kuwa wanapanda miti ili kufanya maeneo yote kuwa ya kijani na pamoja na kuendelea kufanya usafi wa mazingira mara kwa mara ili Dodoma iendelee kung’ara”amesema Mhe.Ndejembi
Aidha Ndejembi, ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote wanao tililisha maji taka kwenye mitaro ilijiengwa maalum kupitisha maji ya mvua.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule ameahidi kusimamia na kuweka mikakati ya usafi katika mifereji.
“Tumesikia maelekezo ya Naibu Waziri aliyoyatoa sisi Dodoma tutalisimamia kwa sababu sheria za mazingira zinafahamika haziruhusu kutupa takataka eneo ambalo sio rasmi,kwa sababu ni chini ya mifereji lazima tuwe na mikakati ya kuhakikisha usafi wa mifereji unafanyika mara kwa mara,
“Kuanzia wiki hii kila mtu tutamfuatilia tuone eneo lake kama ni safi ,na kama ni chafu hatua za kisheria zinatuchukuliwa kama ni faini kama ni chochote tutakifanya,hivyo mwenye eneo lipo chafu aanze kusafisha mwenyewe kabla hatua hazijachukuliwa,na tujenge utamaduni wa kufanya usafi wenyewe,”amesisitiza RC Senyamule
Naye Mkuu wa wilaya ya Bahi Godwin Gondwe, amesema kuwa wameanza kutekeleza maagizo ya serikali ya kuwa na kitalu cha miti na kwa kuanzia wametenga Sh. milioni 20 kwa ajili ya kustawisha miche ya miti na kuipanda katika maeneo mbalimbali.