Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inawaomba wataalam wa afya kutoka Hospitali za Wilaya, Mikoa na Rufaa nchini kuwatuma wagonjwa wenye matatizo ya kuziba kwa mishipa ya damu ya miguu ili watibiwe katika kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya kuzibua mishipa hiyo (Peripheral Interventions).
Kambi hiyo maalum itakayofanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini kuanzia tarehe 19 hadi 21 Juni 2023 itafanywa na madaktari bingwa wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya Andalusia ya nchini Misri ambao watawafanyia wagonjwa upasuaji kwa njia ya tundu dogo kwa kutumia mtambo wa Cathlab.
Aidha tunawaomba wagonjwa wenye matatizo ya kupeleka damu miguuni wafike katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupata matibabu. Huduma hii itakuwa ya kuchangia gharama za matibabu.
Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0754870969 Dkt.George Longopa, 0745836938 Dkt. Dickson Minja na 0788308999 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.
“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.