***********************
NA EMMANUEL MBATILO
Baada ya Mvua kunyesha kwa siku mbili mfululizo katika jiji la Dar es Salaam imesababisha maafa kwa baadhi ya makazi wanaoishi katika maeneo hatarishi ambayo ni Jangwani, Msimbazi Kinondoni Mkwajuni, Tandale na sehemu nyingine nyingi.
Wakizungumza katika nyakati tofauti tofauti wakaz wa maeneo hayo wakilalamika uwepo wa miundo mbinu mibovu ambayo inasabibisha uharibu kujitokeza pindi mvua zitakaponyesha.
Mmoja wa Mkazi wa Msimbazi ambaye ameathirika na maafa hayo Bw.Jofrey Amoni amesema kuwa Serikali ingeongeza juhudi za kutengeneza mifereji katika maeneo ya makzi hatarishi ili kuondokana na Kero hizo.
“Serikali imekuwa ikirekebisha sehemu korofi kwenye maeneo ambayo yanaonekana, ningeomba basi wapite na huku kuangalia wananchi wao tunavyopata shida hasa kwa mvua hizi zinazoendelea kunyesha”. Amesema Bw. Amoni.
Kwa upande wake Rose Shilima mkazi wa Tandale amesema kuwa utupaji wa taka katika mifereji ndo chanzo kikubwa kwa maafa yanayotekea katika maeneo ya Tandale kwani kumekuwa na mifereji mingi kuzibwa maji kushindwa kupita na kufanya maji kuhama njia na kuingia katika makazi ya watu.
“Matukio kama haya yamekuwa yakijitokeza kila mara lakini jamii imekuwa haielewi, wanaambiwa msitupe taka katika mifereji lakini hawasikii, lakini afadhali sasa hata serikali ilivyokataza mifuko ya plastiki kumesaidia kidogo lakini watu hawaelewi”. Amesema Bi. Rose.