Na farida saidy, Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Loata Ole Sanare amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo Mhandisi Emmanuel Kalobelo kuhakikisha anasimamia vyema na kusitisha mara moja swala la watumishi wa Umma kuhamishwa kiholela kutoka maeneo yao ya kazi vijijini na kuhamiashiwa mjini hususani katika sekta ya elimu.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amesema hayo wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Manispaa Ya Morogoro ambapo amemtaka Katibu Tawala huyo kuhakikisha watumishi waliozidi katika maeneo mbalimbali wahamishwe ili kupelekwa vijijini ili kutatua changamoto ya uhaba wa watumishi.
pia Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa watumishi wa idara ya elimu wahakikishe wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba wanapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza huku akiwataka watumishi wa sekta hiyo kuwa tayari kuwapokea wanafunzi hao.
kwa upande wake katibu tawala Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel kalobelo akawata watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu na umoja ili kutatua changamoto zilizopo huku mstahiki meya wa Manispaa ya Morogoro akiwataka watumishi na wananchi kuwa wawazi kwa kila mmoja wao.