Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akihutubia washiriki wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya pili ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET) yaliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha tarehe 22 Mei, 2023.
Sehemu ya washiriki wakifuatailia hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya pili ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET) yaliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha tarehe 22 Mei, 2023.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (katikati) akiwa aomeongozana na viongozi Baraza La Taifa La Elimu Ya Ufundi Na Mafunzo Ya Ufundi Stadi (NACTVET) na Mkoa wa Arusha alipokuwa akitembelea mabanda ya washiriki katika maonesho ya pili ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET) yaliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akizungumza na wanafunzi wenye Ulemavu alipotembelea banda la Arusha City Council Special Education Need na kujionea bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wanafunzi hao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akipata maelezo kutoka kwa washiriki alipotembelea mabanda katika maonesho ya pili ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET) yaliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha tarehe 22 Mei, 2023.
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
Na: OWM (KVAU) – ARUSHA
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi ni muhimu sana katika kuandaa nguvukazi yenye ujuzi unaohitajika katika kuendeleza uchumi wa taifa.
Amebainisha hayo wakati akifunga maonesho ya pili ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET) katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.
Aidha, Naibu Waziri Katambi ameeleza kuwa elimu hiyo itasaidia kuwajenga vijana kuwa na uwezo na ujuzi wa kufanya kazi mbalimbali za kiufundi, kuunda bidhaa na hata kuwa wajasariamali wakubwa.
“Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) ni chombo muhimu katika kusimamia vyuo na kuvifanyia kazi ili viweze kuinua ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi,” amasema
Ameongeza kuwa, Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Saluhu Hassan imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuboresha elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
“Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanza kupitia sera ya elimu ili kuifanya elimu yetu kuwa na tija zaidi na katika mapitio hayo, tunatarajia kuona mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu hapa nchini kwa kuweza kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kuwezesha vijana wetu kuwa na ujuzi unaohitajika,” amesema
Kwa upande mwingine, Naibu Waziri Katambi ametoa wito kwa Waajiri na Wadau wote wa Elimu kushirikiana kwa karibu na Vyuo vya Mafunzo ili viandae Wahitimu wanaohitajika katika soko la ajira.
Naye, Katibu Mtendaji Wa Baraza La Taifa La Elimu Ya Ufundi Na Mafunzo Ya Ufundi Stadi (NACTVET), Dkt. Adolf Rutayuga, amesema kuwa taasisi hiyo itahakikisha inaendelea kutekeleza dhima iliyojiwekea kwa mwaka 2023 ambayo imelenga kuimarisha elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi kwa nguvukazi yenye ujuzi nchini.