Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (nyuma kulia) na mwenzake wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Rahma Kassim Ali wakishuhudia utiaji saini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya ardhi baina ya wizara hizo uliofanywa na makatibu wakuu wa wizara hizo kwenye hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akibadilishana Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kwenye sekta ya ardhi na Dkt. Mngereza Mzee Miraji, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Hamad Abdallah (Kulia) na mwenzake wa Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC) Mwanaisha Ali Said wakionesha Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano wa mashirika hayo mara baada ya kusaini katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati wa utiaji saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya ardhi baina ya wizara yake na ile ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar Rahma Kassim Ali akizungumza katika hafla fupi ya utiaji saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya ardhi baina ya wizara yake na ile ya Tanzania Bara iliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki katika hafla ya utiaji saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya ardhi baina ya wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na ile ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdallah akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya ardhi baina ya wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na ile ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar iliyofanyika jijini Dodoma
Na Gideon Gregory, Dodoma
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angellina Mabula amesema kuwa uwepo wa makubaliano ya mashirikiano baina ya Shirika la Nyumba la taifa (NHC) na lile la Zanzibar (ZHC) utasaidia kuondoa changamoto mbalimbali ikiwemo za makazi bora na upatikanaji wa nyumba bora na za gharama nafuu kwa pande zote mbili.
Dk. Mabula ameyasema hayo leo Mei 20,2023 Jijini Dodoma katika hafla ya utiaji Saini hati za makubaliano ya ushirikiano baina ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (SMT) na Wizara ya Maendeleo ya Makaazi Zanzibar (SMZ).
Amesema wana imani kwa sasa katika huendelezaji wa miji awahitaji kuwa na miji iliyosambaa, wanahitaji kwenda juu kwasababu ardhi inapungua.
“Sasa tukiendelea kuwa na vijumba vya hapa na pale bado tutapata shida, sasa hata kama zinakwenda juu zinakwenda kwa aina zipi ni za makazi au bishara kwahiyo ninyi wenyewe mtasaidia katika hayo,”amesema Dkt. Mabula.
Pia ameongeza kuwa maeneo ya ushirikiano kama yalivyoainishwa katika hati ya makubaliano yaende kufungua ukurasa mpya katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya ardhi, nyumba, maendeleo na makazi.
Amesema ni matarajio yao kupitia hati hizo za makubaliano zitakuwa nyenzo muhimu katika kuleta ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya sekta hiyo pamoja na kuwa na mchango chanya wa kuleta maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
“Tunategemea kila kitakacho kubaliwa hapa basi walau kiingie katika utekerezaji, lengo letu ni kuangalia haya yote tuliyosaini yanatosha na tuongeze wigo mwingine sasa kile mtakacho kisimamia na kukitekeleza katika kipindi hiki kitatusaidia sana,”amesema Dkt. Mabula.
Kwa upande wake Waziri wa ardhi, nyumba, maendeleo na makaazi Zanzibar Rahma Kassim Ali ameomba kuwepo na mpango kazi ili kuhakikisha kile kilichosainiwa kinatekelezeka nak ama kutakuwa na changamoto zitakazojitokeza katika utkelezaji wasikae wenyewe kuzitatua bali waende wazitatue kwa pamoja.
“Pia niseme kwasasa migogoro ya ardhi imekuwa mikubwa, hivyo naamini tukifanikisha jambo hili litaweza kusaidi kutatua masuala haya,”amesema.