Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri( wa pili kutoka kushoto) akiongea na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa kampeni ya chanjo ya surua -rubella .
Waandishi wa habari wa mkoani Tabora wakiwa katika semina ya kuhamasisha chanjo ya surua-rubella inayoanza tarehe 17 Oktoba , 2019
……………..
NA TIGANYA VINCENT
JUMLA ya watoto 489,193 wanatarajiwa kupata chanjo ya surua-rubella mkoani Tabora kuanzia kesho (leo) mkoani Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa (leo)jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa mkutano na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusu kuanza kwa kampeni ya kuzuia na kupambana na magonjwa yanayozuilika.
Alisema kuwa watoto watakaopta chanjo ya surua –rubella ni mwenye umri wa kuanzia miezi 9 hadi miezi 59.
Aidha Mwanri alisema watoto wapatao 213,148 wanatarajia kupata chanjo ya kuzuia polio.
Alisema chanjo hiyo itahusisha watoto wenye umri wa kuanzia miezi 18 hadi 42 kwa Mkoani mzima.
Mwanri alisema lengo mahsusi la kampeni hiyo ni kuzuia na kupambana na magonjwa hayo na kuwaongezea kinga watoto waliokwisha kupatiwa chanjo hizo kwa utaratibu kawaida.
Alitoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya Seikalini , vituo binafsi na vituo vingine vilivyoandaliwa na Halmashauri zore.
Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora (RMO) Dkt. Honarata Rutatinisibwa alitaja madhara yanayoweza kutokea iwapo watoto hawatapata chanjo hizo ni pamoja na kutosikia vizuri na kupata mtoto wa jicho.
Alisema madhara mengine ni mtindio wa ubongo, ukuaji hafifu pamoja na kupooza sehemu za mwili wa mtoto.