Mkurugenzi Mkazi wa USAID Tanzania, Bi.Kate Somvongsiri ,akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa Feed The Future wenye lengo la kuimarisha sekta binafsi (PSSA) hafla iliyofanyika leo Mei 11,2023 jijini Dodoma.
Naibu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Omary Husein,akizungumza wakati akifungua hafla ya uzinduzi wa mradi wa Feed The Future wenye lengo la kuimarisha sekta binafsi (PSSA) hafla iliyofanyika leo Mei 11,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa uzinduzi wa mradi wa Feed The Future wenye lengo la kuimarisha sekta binafsi (PSSA) hafla iliyofanyika leo Mei 11,2023 jijini Dodoma.
Meneja wa Justin Natural Honey Mfugaji wa nyuki,Bw. Justin Mgeni,,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Feed The Future wenye lengo la kuimarisha sekta binafsi (PSSA) hafla iliyofanyika leo Mei 11,2023 jijini Dodoma.
Na Paul Mabeja-DODOMA
SHIRIKA la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) limetoa zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 12 ili kuimarisha ujasiri wa vijana katika sekta za kilimo na kilimo Tanzania.
Mkurugenzi mkazi wa USAID Tanzania, Kate Somvongsiri amesema hayo leo Mei 11, 2023 jijini Dodoma kwenye hafla ya uzinduzi wa maradi wa Feed The Future wenye lengo la kuimarisha sekta binafsi (PSSA).
Amesema, katika kutekeleza programu ya PSSA itaaambatana na kuunga mkono mpango wa wizara ya kilimo wa kujenga kesho bora (BBT).
“Kwa kufanya hivyo PSSA itawafikia vijana 30,000, kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa angalau makampuni 3,000 yanayoongozwa na vijana”amesema
Aidha, amesema shughuli ya kuimarisha sekta binafsi ya Feed The Future Tanzania itatoa ruzuku kwa vyama vya wafanyakazi binafsi,mashirika na makampuni makubwa ambayo yataboresha mazingira wezeshi ya biashra na kupanua fursa za kiuchumi kwa vijana.
“Kwa mafano Khebhandza Marketing Company Limited inapokea ruzuku ya Sh. 287,457,000 kusaidia kuanzisha Malampuni 700 yanayoongozwa na vijana yanayofanya kazi katika sekta ya nafaka,kunde na mbegu za mafuta katika mkoa wa Mbeya na kuunganisha makampuni haya na fedha, huduma na masoko”amesema
Pia, amesema Jumuiya ya wafanyabiashara Wanake Tanzania inapokea ruzuku ya Sh.297,820,024 ili kuanzisha vituo vya biashara,vinavyounganisha biasahra za vijana n autaalam wa kiufundi,huduma za biashara na masoko ya fedha.
“Kupitia PSSA,USAID pia imetoa ruzuku kwa vyama vinavyostahiki,vilivyo n sifam makampuni ya mashirika kwa misingi ya wazai na yenye ushindani”amesema
Kadhalika, amesema kuwa serikali ya Marekani itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuwezesha wananchi wake kufikia uchumi wa kati.
Mmiliki wa Kampuni ya Prano Investment Pendo Ndumbaro,amesema bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mlundikano wa kodi.
“Changamoto nyingine ni vifaa duni kwa ajili ya kuzalishia bidhaa mbalimbali na hii inatokana na ukosefu wa mitaji kwa vijana wafanyabiashara”amesema
Naye Naibu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Omary Husein amesema serikali inatambua umuhimu wa sekta binafasi katika kukuza skta ya kilimo nchini.
“Tunaishukuru sana serikali ya Marekani kupitia shirika lake la USAID kupitia mradi huu utasaidia kuwezesha vijana kupata mitaji ambayo imekuwa kilio chao cha muda mrefu nchini”amesema