Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Tinginya Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma waking’oa mti ili kupisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Tinginya vinavyojengwa kupitia mradi wa kuboresha mazingira ya elimu ya awali na msingi(Boost).
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma Said Bwanali akichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu katika shule ya msingi Tinginya wilaya ni humo.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Tinginya wilayani Tunduru wakichimba msingi ili kuanza rasmi ujenzi wa vyumba vya madasarasa katika shule ya msingi Tinginya wilayani Tunduru.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Julius Mtatiro akichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Tinginya ambapo serikali imetoa zaidi ya Sh.milioni 331.6 kuboresha miundombinu ya elimu kwa shule hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro akizungmza na wakazi wa kijiji cha Tinginya wilayani humo baada ya kushiriki ujenzi wa miundombinu ya elimu katika shule ya msingi Tinginya,Mtatiro amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa miundombinu hiyo na miradi mingine ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita.