Balozi wa Uholanzi nchini, Mh.Wiebe  De Boer, akibadilishana mawazo na Waziri wa Kilimo Mh.Hussein Bashe ,muda mfupi kabla ya kuanza kwa kongamano hilo.

Waziri wa Kilimo Mh.Hussein Bashe. akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa wa Uholanzi nchini,Mh.Wiebe  De Boer baada ya kufungua kongamano la kuendeleza kilimo biashara  nchini.

Wadau wakisikiliza mada wakati wa kongamano hilo

Waziri wa Kilimo Mh.Hussein Bashe. akisalimiana na wadau  mbalimbali waliohudhuria katika kongamano hilo

 

 Sekta ya kilimo bado inazo fursa mbalimbali ambazo zikitumika ipasavyo zitawezesha uchumi wa nchi kukua sambamba na kuzalisha ajira nyingi kwa watanzania.

 Hayo yamebainishwa na Waziri wa Kilimo,Hussein Bashe, wakati akifungua kongamano kuwajengea  uwezo  wakulima kuhusu  kilimo biashara lililoandaliwa na ubalozi wa Uholanzi nchini na kufanyika mjini Dodoma, likiwa linawashirikisha wakulima na wadau mbalimbali katika sekta hiyo.

Kwa upande wake,Balozi wa Uholanzi nchini,Mh. Wiebe  De Boer, alisema Serikali ya nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania hasa katika sekta hiyo ili izidi kukua na kuongeza uchumi.