Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akiaangalia kina cha maji ya Bwawa la Mtera lililopo Mpwapwa Dodoma, wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, ilipotembelea Bwawa hilo ili kuona uwezekano wa kuzalisha zaidi ya lita milioni 133 kwa siku kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa maji katika jiji la Dodoma.
Kaimu Meneja wa Bwawa la Mtera lililopo Mpwapwa Dodoma, Mhandisi Edmund Seif, akieleza jinsi Maji ya Bwawa hilo yanavyotumika kuzalisha nishati ya umeme, wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya maji na Mazingira, ilipotembelea Bwawa hilo kuangalia uwezekano wa Bwawa hilo kuzalisha maji kwa ajili ya matumizi ya wakazi wa jiji la Dodoma
Kamishna wa Mipango ya Kitaifa, Dkt. Mursal Milanzi, akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Mhe. Jackson Kiswaga, wakati wa ziara ya kutembelea Bwawa la Mtera lililopo Mpwapwa Dodoma, ili kuona uwezekano wa kuzalisha zaidi ya lita milioni 133 kwa siku kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa maji katika jiji la Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (kushoto), akiwa katika ziara ya kutembelea Bwawa la Mtera, wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, ilipotembelea Bwawa hilo ili kuona uwezekano wa kuzalisha zaidi ya lita milioni 133 kwa siku kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa maji katika jiji la Dodoma.
Kamishna wa Mipango ya Kitaifa, Dkt. Mursal Milanzi (kulia), akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bw. Benny Mwaipaja, wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, ilipotembelea Bwawa la Mtera, ili kuona uwezekano wa kuzalisha zaidi ya lita milioni 133 kwa siku kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa maji katika jiji la Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, ilipotembelea Bwawa la Mtera lililopo Mpwapwa Dodoma, ili kuona uwezekano wa kuzalisha zaidi ya lita milioni 133 kwa siku kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa maji katika jiji la Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)