WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa,akizungumza kwenye kongamano la kumbukizi ya miaka 101 kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere lililoandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere lililofanyika leo Mei 6,2023 katika Ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda,akielezea jinsi alivyomfahamu Mwalimu Nyerere wakati wa kongamano la kumbukizi ya miaka 101 kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere lililoandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere lililofanyika leo Mei 6,2023 katika Ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Prof. Palamagamba Kabudi ,akitoa mada kuhusu uzalendo uliofanywa na Mwalimu Nyerere wakati wa kongamano la kumbukizi ya miaka 101 kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere lililoandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere lililofanyika leo Mei 6,2023 katika Ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma jijini Dodoma.
Makamu mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Bw.Peter Mavunde,akizungumza wakati wa kongamano la kumbukizi ya miaka 101 kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere lililoandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere lililofanyika leo Mei 6,2023 katika Ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi Maalum Dkt. John Jingu,akizungumza wakati wa kongamano la kumbukizi ya miaka 101 kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere lililoandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere lililofanyika leo Mei 6,2023 katika Ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayoub Rioba,akitoa mada wakati wa kongamano la kumbukizi ya miaka 101 kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere lililoandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere lililofanyika leo Mei 6,2023 katika Ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma jijini Dodoma.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma Prof.Lughano Kusiluka,akitoa mada wakati wa kongamano la kumbukizi ya miaka 101 kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere lililoandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere lililofanyika leo Mei 6,2023 katika Ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wa wakati wa kongamano la kumbukizi ya miaka 101 kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere lililoandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere lililofanyika leo Mei 6,2023 katika Ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 101 ya Kuzaliwa kwa Mwalimu Nyerere wakimsikiliza Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa (hayupo pichani) ,akizungumza kwenye kongamano la kumbukizi ya miaka 101 kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere lililoandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere lililofanyika leo Mei 6,2023 katika Ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa ,ameziagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kuandaa utaratibu utakaosaidia vijana kujifunza na kumfahamu Mwalimu Nyerere.
Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo kwenye kongamano la kumbukizi ya miaka 101 kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere lililoandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere lililofanyika leo Mei 6,2023 katika Ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma.
Majaliwa amesema kuwa kuna mambo ambayo vijana wanapaswa kufahamu ikiwamo kumfahamu na kumuelezea Mwalimu Nyerere, kipaji chake katika harakati za kupigania uhuru, kutambua juhudi katika harakati za kuleta amani,kuimarisha ustawi wa Tanzania,maisha ya Nyerere.
Amesema kuwa katika uhai wa Mwalimu katika uongozi wake alisisitiza masuala kama urithi na falsafa zake, alisisitiza kupinga ukabila alikemea kila wakati, udini ni jambo alisisitiza na kuasa viongozi wasitafute uongozi kwa kigezo cha udini.
“Tusiingie huko kwenye masuala ya ukabila na udini, jambo jingine kupambana na ujinga, maradhi na umasikini, maadili ya uongozi na kupinga rushwa, alisisitiza Mwalimu viongozi safi wasiopenda rushwa na rushwa ndio adui wa maendeleo yetu,”amesema Mhe.Majaliwa
Hata hivyo amesema kuwa katika harakati za kisiasa za Mwalimu alitamani kuunganisha nchi na kuwa na uongozi wa pamoja na ndio mafanikio ya Tanganyika na Zanzibar.
“Tunashuhudia falsafa zake zinaishi na ni jukumu letu sisi kuyaendeleza ili vizazi vijavyo viishi na falsafa hizi, taasisi hii haifungamani na itikadi yeyote ya siasa lengo ni kuendeleza umoja, ustawi wa watanzania,”amesema
Aidha ameipongeza Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambayo inalenga kuwafikia vijana ili kuwa na uelewa mpana kazi zilizofanywa na waasisi.
“Madhumuni ya kongamano hili ni kurithisha fikra na falsafa za Mwalimu kupitia kumbukizi hii zitazinduliwa klabu za mazingira za Mwalimu Nyerere kwenye vyuo, shule za msingi na sekondari, napongeza taasisi kwa hatua hii,”amesema
Pia Waziri Mkuu ametoa wito kwa mamlaka mbalimbali kushirikiana na taasisi hiyo katika kutoa elimu ya falsafa ya Mwalimu Nyerere, uzalendo na juhudi hizo zitachangia kupambana na maovu ikiwamo rushwa.
Hata hivyo, Mhe.Majaliwa amesema, kumejitokeza taharuki kwa baadhi ya viongozi wa dini wakati Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linashughulikia malalamiko kuhusu ongezeko la kelele na mitetemo.
“Serikali ingependa kutoa ufafanuzi kwamba shughuli za dini ziendelee kufanyika kama kawaida na suala la uratibu wa jambo hilo katika nyumba za ibada liendelee kuratibiwa na viongozi wa dini wenyewe kupitia Jumuiya ya Maridhiano na Amani.”
“Serikali itaendelea kushauriana na jumuiya ya maridhiano na amani katika kuona namna bora ya kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia mahitaji ya jamii na kulinda afya za Watanzania,” amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, amesema alitumikia Ofisi binafsi ya Mwalimu Nyerere kutokana na uzalendo na nidhamu ya maisha.
“Jambo nililiona kwa Mwalimu ni hofu ya Mungu, usidhani kama umesoma basi Mungu hayupo we kijana wewe, nguvu yako ipo wapi nendeni kanisani na misikitini msali, ni zuri kwa maisha yenu,”amesema Mhe.Pinda
Awali Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mzee Paul Kimiti ameiomba Serikali itenge eneo kwa ajili ya makumbusho ya hayati Mwalimu Nyerere katika makao makuu ya Serikali hapa Dodoma ambayo yatahifadhi historia yake.
“Nataka Dodoma iwe mahali pa utalii waangalie historia ya Baba wa Taifa, tunataka tupate eneo la zaidi ya hekari 300 ili taasisi mbalimbali ziweke vitu vyake, kuwe na mifugo, wanyama, michezo tunataka iwe mahali pa utalii, tumeona wazee tuliseme mapema hatutatumia fedha za serikali wapo wafadhili watatoa,”amesema
Akitoa mada, Mbunge wa Kilosa, Prof.Palamagamba Kabudi amesema vijana wanapaswa kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo na kupambana na kila aina ya nyufa zinazotaka kuvuruga umoja, amani na nchi.
Naye Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu, amewahimiza vijana kushika maadili na utamaduni wa kitanzania.