Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima
(kulia), akimfafanulia jambo Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola (kushoto),
wakati walipotembelewa na Balozi wa Ethiopia Nchini, Yonas Yosef Sanbe, Ofisi
za Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ethiopia Nchini, Yonas Yosef Sanbe, baada ya Balozi huyo
kuwatembelea viongozi hao, jijini Dodoma, leo. Picha zote na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima
(kulia) akimuaga Balozi wa Ethiopia nchini, Yonas Yosef Sanbe, baada ya Balozi
huyo kumaliza mazungumzo na Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola (hayupo
pichani), jijini Dodoma, leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima
(kulia), akimfafanulia jambo Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola (kushoto),
wakati walipotembelewa na Balozi wa Ethiopia Nchini, Yonas Yosef Sanbe, Ofisi
za Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akizungumza na
Balozi wa Ethiopia nchini, Yonas Yosef Sanbe, masuala mbalimbali ya ushirikiano
kati ya Nchi ya Ethiopia na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika Ofisini kwa
Waziri huyo, jijini Dodoma, leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
**************************
Na Felix Mwagara, MOHA, Dodoma.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya mazungumzo na
Balozi wa Ethiopia nchini, Yonas Yosef Sanbe na kumuhakikishia ushirikiano
zaidi kati ya Wizara yake na Ubalozi huo nchini.
Mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Lugola,
jijini Dodoma, leo, ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa
ushirikiano kati ya Tanzania na Ethiopia.
Waziri Lugola alimuhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuwa
salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini.
“Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola.
Kwa upande wake Balozi Sanbe, alimshukuru Waziri Lugola kwa mazungumzo
waliyoyafanya na kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Ethiopia na Tanzania.