WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,akizungumza wakati akifungua mafunzo ya wabunge yaliyoandaliwa na Wizara ya Maji yenye lengo la kueleza sekta hiyo na mikakati ya Wizara katika kuwapelekea maji wananchi bungeni jijini Dodoma.
SPIKA wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson,akizungumza wakati wa mafunzo ya wabunge yaliyoandaliwa na Wizara ya Maji yenye lengo la kueleza sekta hiyo na mikakati ya Wizara katika kuwapelekea maji wananchi bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso,akizungumza wakati wa mafunzo ya wabunge yaliyoandaliwa na Wizara yake yenye lengo la kueleza sekta hiyo na mikakati ya Wizara katika kuwapelekea maji wananchi bungeni jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Cyprian Luhemela,akielezea mikakati ya Wizara katika kufikisha maji kila sehemu wakati wa mafunzo ya wabunge yaliyoandaliwa na Wizara hiyo yenye lengo la kueleza sekta hiyo na mikakati ya Wizara katika kuwapelekea maji wananchi bungeni jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia mafunzo ya wabunge yaliyoandaliwa na Wizara ya Maji yenye lengo la kueleza sekta hiyo na mikakati ya Wizara katika kuwapelekea maji wananchi.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa , amesema wabunge wana matumaini na Wizara ya Maji kuwa mpango kazi walioweka wa kuhakikisha wanafikisha maji maeneo yote nchini na kutunza vyanzo vya maji.
Waziri Mkuu ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya wabunge yaliyoandaliwa na Wizara ya Maji yenye lengo la kueleza sekta hiyo na mikakati ya Wizara katika kuwapelekea maji wananchi.
“Kutokana na umuhimu huo ndio maana wizara imekuja hapa kutueleza nini inafanya kutekeleza suala hilo, na kila mamlaka za maji zimepewa kazi ya kusimamia miradi ya maji na kazi nzuri inaendelea,”alisema Majaliwa.
Aidha amesema wizara imeamua kuja kueleza nini inafanya ili huduma hiyo ipatikane kwa urahisi huku akieleza ana matumaini na wizara kuwa mpango watakaokuja nao utaondoa changamoto ya maji kwenye maeneo yenye uhitaji.
Hata hivyo Waziri Mkuu ameipongeza Wizara kwa kazi nzuri inayofanya nchini kwa kutekeleza miradi mingi ambayo faida inaonekana kwa wananchi kupata huduma hiyo.
“Namshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutoa maelekezo ya nini kifanyike kuhusu utoaji huduma za maji nchini ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM,”alisema Majaliwa.
Kwa upande wake Waziri wa Maji Jumaa Aweso aliwaahidi wabunge kuwa wizara haitakuwa kikwazo kwenye utaoji huduma ya maji ili kutimiza lengo la Rais la kumtua mama ndoo kichwani.
Awali Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Cyprian Luhemela alisema Tanzania haina changamoto ya vyanzo vya maji bali usambazaji wa huduma hiyo.
Alifafanua Tanzania bara ina jumla ya vijiji 12,312 na katika mwaka wa fedha 2022/23 serikali imekamilisha miradi 594 kwenye vijiji 1,173 ambayo imeongeza idadi ya watu 3,480,289.
“Kwa sasa wananchi 30,209,409 sawa na asilimia 77 ya watanzania wote waishio vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama,”alisisitiza Mhandisi Luhemela.