Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani alhaj Abubakar Kunenge, amezindua Daraja la Mipeko lililopo barabara ya Mwanambaya lenye thamani ya sh. Milion 214.
Akisalimia Wananchi wa Mipeko Kunenge alisema, mkoa huo una mtandao wa barabara wa km 6629 zinazohudumiwa na Wakala wa barabara TANROADS na TARURA.
Alieleza, bajeti ya kutekeleza shughuli za barabara kwa mwaka 2021/22 ilikuwa ni bilioni 75.5 na kwa mwaka 2022/23 imeongezwa kufikia bilion 81.
Kunenge,aliwataka wananchi wa eneo hilo kulinda Daraja hilo kwa manufaa ya muda mrefu.
Vilevile alitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga kupanga Mji wa Mkuranga kwa kuwa Mji huo unakuwa kwa kasi.
Kunenge alieleza, Serikali inafanyia kazi maombi ya Wananchi hao ya kujengewa Kituo cha Afya, kupelekewa Umeme na ujenzi wa Daraja.
“Nampongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Maendeleo ambayo yanamgusa Mwanachi wa kawaida,na kutanua mtandao wa barabara ili kuondoa changamoto za miundombinu kwa Wananchi “
Anaeleza Rais alipofanya ziara Mkoani Pwani alieleza nia yake ya kuhakikisha Mkoa huo unapata Miundombinu ya yote Muhimu ya Afya, Elimu, Maji, Nishati, Barabara,na kazi inaonekana na inaendelea.