Na Victor Masangu,Kibaha
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha mji Elina Mgonja amewahimiza wanawake kushikamana kwa pamoja kwa lengo la kukiimarisha chama ili kiweze kushinda katika chaguzi zake mbali mbali ikiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka 2024.
Mgonja ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea wanachama viongozi wa mbali mbali wa ccm ikiwemo pamoja na kuzungumza nao ili kubaini changamoto zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba lengo lake kubwa ya kufanya ziara hiyo ni kwa ajili ya kukiimarisha chama pamoja na kupata taarifa mbali mbali za utekelezaji wa Ilani ya chama.
Pia aliwaasa viongozi mbali mbali wa ccm katika ngazi zote pamoja na kuwahimiza viongozi wa serikali za mitaa Kuhakikisha wanahudhulia katika vikao mbali mbali ili kuweza kutambua mambo ambayo yametekelezwa katika maeneo yao.
Kadhalika aliwaomba viongozi kuwa na utamaduni wa kuyasemea mambo ambayo yanatekelezwa na madiwani pamoja na kazi za maendeleo ambazo zinafanywa na Mbunge wa kibaha mjini Silvestry Koka.
“Kwa Sasa inabidi tujipange kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo viongozi wenzangu inatakiwa kushikamano kwa pamoja ili tuweze kusinda kwa kishindo katika uchaguzi huo bila kupoteza nafasi hata moja,”alisema Mngonja.
Kadhalika alimpongeza mlezi wa UWT Selina Koka kwa kuweza kuwasaidia wanawake katika nyanja mbali mbali ikiwemo kiuchumi na kuwaondoa katika wimbi la umasiki.
Kwa upande mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Selina Koka ambaye pia ni mlezi wa umoja huo alibainisha kuwa ataendelea kuwasaidia kwa hali na mali ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Ziara ya Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mji pamoja na kamati ya utekelezaji imewajumuisha viongozi mbali mbali wa chama pamoja na jumuiya zake lengo kubwa ikiwa ni kukiimarisha chama ili kiweze kushinda katika chaguzi mbali mbali.