Wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao kutoka Shirika la Madaktari Africa la nchini Marekani kumfanyia upasuaji wa tundu dogo kwa kutumia mtambo wa Cath lab mgonjwa mwenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu hayo leo jijini Dar es Salaam. Wagonjwa 10 wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi hiyo.
Wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani wakiangalia umeme wa moyo unaoingia kwa mgonjwa unavyofanya kazi kwa kutumia mashine ya CRTD Programmer wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu hayo leo jijini Dar es Salaam. Wagonjwa 3 kati ya 10 wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo wameshafanyiwa upasuaji katika kambi hiyo.