Na Victor Masangu,Kibaha
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ametekeleza ahadi yake kwa vitendo kwa kuamua kuchangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kuanza ujenzi wa ofisi za Bakwata Wilaya ya Kibaha.
Koka ameyasema hayo wakati wa Baraza kuu la Eid Wilaya ya Kibaha ambalo lilifanyika katika viwanja vya shule ya msingi kongowe na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa kiislamu kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Mkoa.
Mbunge huyo alisema kwamba amekuwa kushirikiana bega kwa bega na Baraza kuu la waislamu kuanzia ngazi ya Wilaya kwa kipindi kirefu tangu mnamo mwaka 2015 na kwamba amechangia mifuko hiyo ikiwa ni moja ya utekelezaji wa ahadi yake kwa vitendo.
“Mimi Kama Mbunge katika kipindi Cha Baraza lililopita nilipokea maombi kuhusu ukosefu wa kuwa ña ofisi ya Bakwata Wilaya ya Kibaha kwa hivyo nikawaambia watafute eneo kwa ajili ya ujenzi na leo nimefurahi kwani nimekwenda kulitembelea na ndio maana nimeanza na mifuko 100,,”alisema Koka.
Pia Koka pia katika Baraza hilo aliungwa mkono na mjumbe wa halmashauri ya ya chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Mansoor Musa ambaye na yeye kuchangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo.
Katika hatua nyingine Koka aliwaasa wawazi na walezi Kuhakikisha wanaweka misingi imara katika kuendelea kuzilinda mila na desturi pàmoja na kuimarisha maadili katika jamii inayotuzunguka.
Kwa Upande wake kaimu Sheikh Zuberi Chamgunda alimpongeza kwa dhati Mbunge Koka kwa kushirikiana na jamii kwa hali na mali ikiwemo kutekeleza ahadi yake ya kuchangia mifuko 100 ya saruji.
Nao baadhi ya waislamu ambao walishiriki katika Baraza hilo la Eid walisema kuwa kupatikana kwa ofisi ya Bakwata Wilaya itakuwa ni mkombozi kwao hivyo wamewaomba wadau wengine kuiga juhudi za Mbunge Koka kujitolea kwa moyo katika shughuli za kijamii.