Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akishiriki Ibada ya Jumapili katika Nyumba ya Malezi ya Mtakatifu Yosefu iliopo Miyuji Jimbo kuu katoliki Dodoma leo tarehe 23 Aprili 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na waumini waliohudhuria Ibada ya Jumapili katika Nyumba ya Malezi ya Mtakatifu Yosefu iliopo Miyuji Jimbo kuu katoliki Dodoma leo tarehe 23 Aprili 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Padre Stanslaus Mitti pamoja na Masista mbalimbali wa kituo cha kulea watoto yatima cha Nyumba ya Matumaini Miyuji mara baada ya Ibada ya Jumapili katika Nyumba ya Malezi ya Mtakatifu Yosefu iliopo Miyuji Jimbo kuu katoliki Dodoma leo tarehe 23 Aprili 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa na Padre Stanslaus Mitti katika picha ya pamoja watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Nyumba ya Matumaini-Miyuji kinachoendeshwa na Masista wa Moyo Mtakatifu wa Yesu Mteswa mara baada ya Ibada ya Jumapili katika Nyumba ya Malezi ya Mtakatifu Yosefu iliopo Miyuji Jimbo kuu katoliki Dodoma leo tarehe 23 Aprili 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa waumini na viongozi wa dini hapa nchini kuendelea kuwaombea viongozi wa serikali ili waweze kuongoza taifa vile inavyompendeza Mungu.
Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe 23 Aprili 2023 wakati akiwasalimu waumini mara baada ya Ibada ya Jumapili iliofanyika katika Nyumba ya Malezi ya Mtakatifu Yosefu iliopo Miyuji Jimbo kuu katoliki Dodoma leo tarehe 23 Aprili 2023, ibada ilioongozwa na Padre Stanslaus Mitti. Dkt. Mpango amesema ni vema kuendelea kuiombea nchi ipate kuwa na amani wakati wote pamoja na viongozi na watumishi wa taifa waweze kutenda kazi kwa hekima ya Mungu.
Vilevile Makamu wa Rais amewakumbusha waumini na watanzania kwa ujumla umuhimu wa malezi kwa watoto na vijana kuanzia nyumbani. Amesema ni vema wazazi wakafanya kazi ya ziada katika kufuatilia mienendo ya watoto na vijana,wakike kwa wakiume mahali popote ikiwemo vyuoni.
Halikadhalika, Makamu wa Rais ametoa wito kwa waumini wa kanisa hilo na wananchi wa Dodoma kuongeza jitihada katika usafi wa mazingira, kupanda miti na maua na kuepukana na tabia za kutupa taka ovyo katika maeneo yao. Amesema Mwenyezi Mungu ameijaalia Tanzania mazingira mazuri hivyo hakuna budi kuitunza kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.