MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule,akizungumza katika kikao cha kujadili mradi wa BOOST na Wakuu wa Wilaya, Maafisa Elimu na Wakurugenzi wa Jiji la Dodoma kilichofanyika ofisini kwake.
SEHEMU ya Wakuu wa Wilaya, Maafisa Elimu na Wakurugenzi wa Jiji la Dodoma wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kujadili mradi wa BOOST kilichofanyika Ofisini Kwake jijini Dodoma.
Na Gideon Gregory, Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule amesema kuwa Zaidi ya shilingi Bilioni 6 zimetengwa ili kukamilisha ujenzi wa shule mpya za msingi 16 katika mkoa huo.
Mh. Senyamule ameyasema hayo Aprili 21, katika kikao cha kujadili mradi wa BOOST na Wakuu wa Wilaya, Maafisa Elimu na Wakurugenzi wa Jiji la Dodoma kilichofanyika ofisini kwake.
Amesema vyumba vya madarasa 153 vitajengwa ambapo zaidi ya Bilioni 3 zimetengwa kuhakikisha yanakamilika.
“Madarasa ya mfano Elimu ya awali 16 yatajengwa na kiasi cha fedha cha shilingi 508,800,000.00 zimetengwa, Darasa la elimu maalum moja litajengwa ambapo shilingi 23,000,000.00 zimetengwa Pamoja na matundu ya vyoo 106 yakitarajiwa kujengwa shilingi 180,200,000.00 zimetengwa ,”amesema Mhe Senyamule
Aidha ameongheza kuwa kupitia mradi wa SEQUIP Zaidi ya bilioni 5 zilipokelewa kwaajili ya ujenzi wa shule mpya 11 za sekondari ambapo kila shule ilipata zaidi ya milioni 4 kwa shule za Mpingwa (Bahi), Mtemi Chiloloma (Jiji), Keikei (Kondoa DC), Tura day (Kondoa Mji), na Lenjulu (Kongwa) na ujenzi wake umekamilika.
Amesema mradi huo ni wa mwaka 2021/2022 na ujenzi bado unaendelea kwa shule za Lwondo (Mpwapwa), Zajilwa (Chamwino), Nhinhi (Chamwino) na Churuku (Chemba) huku ukiwa bado unahitaji usimamizi wa karibu ili ukamilike.