Mkurungezi mkuu wa kamapuni Kampuni ya ununuzi wa zao la tumbaku ya Mkwawa Tobacco Leaf Matthew Kapnias akikabidhi mfuko wa Sukari kaimu mkuu wa Gereza kuu wa Uyui, Mrakibu Mwandamizi wa jeshi la Magereza Richard Malifedha wengine katika picha ni Shekh wa Mkoa wa Tabora Ibrahimu Mavumbi na Mkurungezi mkuu wa msaidizi wa kampuni hiyo Richard Sinamtwa.
Mkurungezi mkuu wa kamapuni Kampuni ya ununuzi wa zao la tumbaku ya Mkwawa Tobacco Leaf Matthew Kapnias akikabidhi Ndoo ya mafuta ya kupikia kwa mkuu wa Gereza la Mahabusu Mrakibu Mwandamizi wa jeshi la Magereza, Ally Lipululu.
Masista wa huruma wa kituo cha kulelea watoto yatima cha mama Tereza Manispaa ya Tabora wakipokea katoni ya Sabuni kutoka kwa Mkurungezi mkuu wa kamapuni Kampuni ya ununuzi wa zao la tumbaku ya Mkwawa Tobacco Leaf Matthew Kapnias.
Msimamizi wa kituo cha watoto yatima cha Igambilo Ophans Centre Abdulhamiid Willah Akipokea Ndoo ya Mafuta kutoka kwa Mkurungezi mkuu wa kamapuni Kampuni ya ununuzi wa zao la tumbaku ya Mkwawa Tobacco Leaf Matthew Kapnias.
Picha ya pamoja kati ya viongozi wa kampuni ya ununuzi wa zao la tumbaku ya Mkwawa Tobacco Leaf wakiongozwa na mkurungezi mkuu Matthew Kapnias na Maafisa wa jeshi la Magereza wakiongozwa na kaimu mkuu wa Gereza kuu wa Uyui, Mrakibu Mwandamizi wa jeshi la Magereza Richard Malifedha.
Picha ya Pamoja kati ya Masista wa huruma wa kituo cha kulelea watoto yatima cha mama Tereza wakiongozwa na Sista Jenny Charenty pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo hicho .
Na Lucas Raphael,Tabora
Kampuni ya ununuzi wa zao la tumbaku ya Mkwawa Tobacco Leaf mkoani Tabora limetoa vifaa mbalimbali na sadaka kwa vituo viwili vya watoto yatima na Magereza vitu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 20,445,000/
Akizungumza wakati wa utoaji wa vifaa hivyo na sadaka hiyo mkurungezi mkuu wa kamapuni hiyo Matthew Kapnias alisema kwamba wametoa kwa ajili ya watu wenye uhitaji iliiweze kuwasaidia katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Alisema kwamba uongozi wa kampuni hiyo uliona kuna umuhmu wa kufanya hivyo kwa vikundi hivyo na kuisaidia serikali kuwapatia sadaka kwa wahitaji waliomo kwenye taasisi hizo za kijamii.
Alitaja vitu vilivyotolewa ni Mchele kilo 3000,Sukari mifuko 50,Mafuta ndoo 20,Sabuni katoni 50, Karanga kilo 125 na wembe dazani 400.
Alivuitaji vitu vingine kuwa ni Magodoro 115 ,Mashuka 280 Na Neti 185.
Mkurungezi mkuu wa msaidizi wa kampuni hiyo Richard Sinamtwa akitoa ufafanuzi wa vitu vilivyolewa kwenye Gereza kuu la Uyui mkoani hapa,alisema kwamba lilipatiwa Mchele mifuko 25,Sukari mifuko 10 mafuta Ndoo 3 Sabuni bosi 10,Karanga kilo 75 na wembe .
Alisema kwamba katika Gereza la mahabusi walipatiwa Mchele mifuko 10,Sukari mifuko 4 Mafuta ndoo 3 ,Sabuni Bosi 10 na Karanga kilo 50.
Sinamtwa alisema kwamba Sadaka hiyo imetolewa kwa ajili ya Futari kwa wafungwa waliofungwa ndani ya magereza hayo na kuwapatia faraji kuona jamii inawakumbuka .
Wakipokea Sadaka hiyo kaimu mkuu wa Gereza kuu wa Uyui, Mrakibu Mwandamizi wa jeshi la Magereza Richard Malifedha na mkuu wa Gereza la Mahabusu Mrakibu Mwandamizi wa jeshi la Magereza, Ally Lipululu walishukuru kwa kutoa Sadaka hiyo kwa wafungwa waliopo ndani ya magereza hayo nakuomba misaada hiyo isiishie leo bali waendeleea kutoa zaidi kwa magereza wahitaji sana misaada hiyo .
Hata hivyo Sinamtwa pia alisema kwamba walitoa msaada katika kituo cha Masista wa huruma cha mama Tereza ambapo walitoa Magodoro 40,Neti 50 ,Mashuka 90 Sukari mifuko 10,Mchele mifuko 15, Mafuta ndoo 3 Sabuni katoni 5.
Aidha alisema kituo cha watoto yatima cha Igambilo Ophans Centre akilipatiwa Magodoro 45,Neti 75 ,Mashuka 90 Sukari mifuko 10,Mchele mifuko 25, Mafuta ndoo 3 Sabuni katoni 10.
Akipokea msaada huyo Sista Jenny Charenty alisema kwamba wanaishukuru kampuni hiyo ya Tumbaku kwa kutoa misaada hiyo kwani imekuja kipindi ambacho walikuwa wanauhitaji mkubwa wa Neti na chakula .
Naye Msimamizi wa kituo cha watoto yatima cha Igambilo Ophans Centre Abdulhamiid Willah alishukuru kupata misaada hiyo kwani kampuni hiyo imetafasiri maneno ya mtume kwa vitendo cha kuwajali na kuwathamini watoto yatima na wajane.