NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.
MBUNGE wa Jimbo la Amani, Zanzibar Mhe.Abdul Yussuf Maalim ametoa wito kwa viongozi wa mashina hadi jimbo kutoa ushirikiano kwa pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo katika jimbo hilo.
Abdul alitoa wito huo wakati akitoa sadaka ya mwezi Mtukufu ramadhani kwa mabalozi na wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo hilo katika ofisi za CCM Wilaya ya Amani mjini Unguja, Zanzibar.
Akizungumza na viongozi hao baada ya kutoa sadaka hiyo, Abdull ambaye alichaguliwa Desemba mwaka jana kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Mussa Hassan Mussa, pia aliwashukuru wananchi na viongozi hao kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo.
“Tangu nilipochaguliwa miezi miwili sasa nilikuwa sijapata muda wa kuwashukuru, kwahiyo mbali na kutoa sadaka hii lakini nimeona nitumie fursa hii kuzungumza nanyi na kutoa shukrani zangu za dhati kutokana na imani yenu mlioionyesha kwangu kunichagua kwa kishindo,”
Alitumia fursa hiyo kuwaomba wampe ushirikiano wa karibu zaidi kila mmoja kwa nafasi yake ili waweze kufanya kazi kwa pamoja kutekeleza ilani ya chama na kupata maendeleo kwa ajili ya jimbo hilo.
“Niwaombe sana wazee wangu, msinitupe hizi ni nafasi tu lakini kwa umoja wetu tuendelee kushikamana kwa pamoja tusonge mbele,” alisema
Nao baadhi ya viongozi hao pamoja na kumshukuru kwa sadaka aliyoitoa kwao, walimuahidi mbunge huyo kuendelea kutoa ushirikiano ili kuleta mabadiliko zaidi katika jimbo hilo.
Omar Abdala Kassim alisema watazidi kushirikiana kutataua changamoto za wananchi “kubwa zaidi tuendele kuombeana kupata neema zaidi.
Naye Khadija Saleh alisema wanatakiwa kushikamana katika itazamo ya kisiasa kidini na kijamii na kuendelza umoja wao