Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Abdulrahman Kinana akifunga mafunzo ya muda mfupi ya uongozi kwa vijana 74 wanaotoka katika vyama  Vyenye Ushirikiano wa Pamoja na  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania ambavyo ni ANC Cha  afrika kusini, SWAPO Cha  Namibia,  ZANU- PF Cha Zimbabwe, FRELIMO Cha Msumbiji na MPLA  Cha Angola
Washiriki wa  mafunzo ya muda mfupi ya uongozi wakisikiliza hotuba ya Ufungaji Vijana hao  wanaotoka katika vyama  Vyenye Ushirikiano wa Pamoja na  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania ambavyo ni ANC Cha  afrika kusini, SWAPO Cha  Namibia,  ZANU- PF Cha Zimbabwe, FRELIMO Cha Msumbiji na MPLA  Cha Angola.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Abdulrahman Kinana akigawa Vyeti kwa Wahiriki wa  mafunzo ya muda mfupi ya uongozi  wanaotoka katika vyama  Vyenye Ushirikiano wa Pamoja na  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania ambavyo ni ANC Cha  afrika kusini, SWAPO Cha  Namibia,  ZANU- PF Cha Zimbabwe, FRELIMO Cha Msumbiji na MPLA  Cha Angola. 
 
Washiriki wa  mafunzo ya muda mfupi ya uongozi Wakiimba nyimbo wakati wa Ufungaji wa mafunzo ya Vijana hao  wanaotoka katika vyama  Vyenye Ushirikiano wa Pamoja na  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania ambavyo ni ANC Cha  afrika kusini, SWAPO Cha  Namibia,  ZANU- PF Cha Zimbabwe, FRELIMO Cha Msumbiji na MPLA  Cha Angola. (PICHA NA FAHADI SIRAJI)
 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana,ametoa rai kwa vyama sita vilivyoshiriki katika harakati za ukombozi kusini mwa Afrika kuendelea kuwapa mafunzo viongozi vijana kwa lengo la kuwaandaa wawe bora kwa ustawi wa vyama na mataifa yao kwa ujumla.
 
Amesema anaamini vijana  wakipata mafunzo  yatawaanda kushika uongozi katika sekta mbalimbali za mataifa yao na yatawasaidia  kuongeza uwelewa na kuleta matokeo chanya.
 
Kinana aliyasema hayo jana  wakati akifunga programu ya mafunzo kwa viongozi vijana, kutoka vyama sita vya  wapigania uhuru nchi za kusini  mwa Afrika.
 
“Kazi ya kuwalea vijana ni pamoja na kuwafunza, kuwasamehe  pale wanapokosea , kuwasahihisha ili wapate taaluma ya uongozi na kuwa viongozi bora wa kuongoza wananchi wa nchi zetu.
 
“Tuache kutumia lugha kuwa vijana ni taifa la kesho, vijana sio taifa la kesho, vijana ni viongozi wa leo lazima tuwape nafasi ya kuongoza,”alisema
 
Alisema asilimia 70 ya Watanzania na nchi nyingi Afrika ni vijana na ni viongozi wa sasa hivyo ni vyema waaminiwe na kupatiwa nafasi  ya kuongoza. 
 
Pia Kinana alishukuru Chama Cha Kikomonisti cha China (CPC) kwa kuendelea ushirikishiana na vyama hivyo, huku akisema CCM itaendelea kudumisha umoja na ushirikiano baina ya vyama it it vyote.
 
Vyama vilivyoshiriki katika katika mafunzo hayo CCM kutoka Tanzania, SWAPO kutoka Namibia, MPLA kutoka Angola, ZANU PF kutoka  Zimbabwe , ANC Afrika Kusini na FRELIMO kutoka Msumbiji.