MKURUGENZI wa Huduma ya Uuguzi na Ukunga Tanzania kutoka Wizara ya Afya Bi.Ziada Sellah,akizungumza wakati wa Madhimisho ya Siku ya Usonji Duniani yaliyofanyika Kitaifa leo Aprili 2,2023 Jijini Dodoma.
MKURUGENZI wa Huduma ya Uuguzi na Ukunga Tanzania kutoka Wizara ya Afya Bi.Ziada Sellah,akiongoza maandamano wakati wa Madhimisho ya Siku ya Usonji Duniani yaliyofanyika Kitaifa leo Aprili 2,2023 Jijini Dodoma.
MKURUGENZI wa Huduma ya Uuguzi na Ukunga Tanzania kutoka Wizara ya Afya Bi.Ziada Sellah,akizungumza wakati wa Madhimisho ya Siku ya Usonji Duniani yaliyofanyika Kitaifa leo Aprili 2,2023 Jijini Dodoma.
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe ,akizungumza wakati wa Madhimisho ya Siku ya Usonji Duniani yaliyofanyika Kitaifa leo Aprili 2,2023 Jijini Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Dk.Paul Lawala,akizungumza wakati wa Madhimisho ya Siku ya Usonji Duniani yaliyofanyika Kitaifa leo Aprili 2,2023 Jijini Dodoma.
MKUU wa Shule ya Msingi Mlezi Mwl Anisetus Lyimo,akielezea changamoto ambayo inawakabili katika shule yake wakati wa Madhimisho ya Siku ya Usonji Duniani yaliyofanyika Kitaifa leo Aprili 2,2023 Jijini Dodoma.
AFISA Elimu Maalumu Jiji la Dodoma Mwl Issa Kambi,akizungumza wakati wa Madhimisho ya Siku ya Usonji Duniani yaliyofanyika Kitaifa leo Aprili 2,2023 Jijini Dodoma.
AFISA Kitengo cha Elimu Maalumu anayeshughulikia Usonji kutoka TAMISEMI Bi.Agnes Mwingira,akizungumza wakati wa Madhimisho ya Siku ya Usonji Duniani yaliyofanyika Kitaifa leo Aprili 2,2023 Jijini Dodoma.
AFISA Kitengo cha Elimu Maalumu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Bi.Ahiadu Sangoda,akizungumza wakati wa Madhimisho ya Siku ya Usonji Duniani yaliyofanyika Kitaifa leo Aprili 2,2023 Jijini Dodoma.
MWANZILISHI na Mkurugenzi Mtendaji wa Lukiza Austism Foundation Bi.Hilda Nkabe,akizungumza wakati wa Madhimisho ya Siku ya Usonji Duniani yaliyofanyika Kitaifa leo Aprili 2,2023 Jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotubaya Mkurugenzi wa Huduma ya Uuguzi na Ukunga Tanzania kutoka Wizara ya Afya Bi.Ziada Sellah,(hayupo pichani) wakati wa Madhimisho ya Siku ya Usonji Duniani yaliyofanyika Kitaifa leo Aprili 2,2023 Jijini Dodoma.
MKURUGENZI wa Huduma ya Uuguzi na Ukunga Tanzania kutoka Wizara ya Afya Bi.Ziada Sellah,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua mwezi wa kampeni ya uelewa ugonjwa wa usonji duniani wakati wa Madhimisho ya Siku ya Usonji Duniani yaliyofanyika Kitaifa leo Aprili 2,2023 Jijini Dodoma.
Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imejipanga kuzalisha walimu wengi watakaoweza kuwafundisha wanafunzi wenye ugonjwa wa Usonji kwa kuanzisha mafunzo ya Diploma katika vyuo mbalimbali nchini.
Hayo yameelezwa leo Aprili 2,2023 Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Huduma ya Uuguzi na Ukunga Tanzania kutoka Wizara ya Afya Bi.Ziada Sellah, kwenye uzinduzi wa mwezi wa kampeni ya uelewa ugonjwa wa usonji duniani.
Bi.Ziada amesema kwa sasa watoto wapatao 1416 wenye ugonjwa huo wamesajiliwa katika shule 18 ambapo kuna walimu 157.
”Katika kukabiliana na tatizo hilo la idadi ndogo ya walimu,shule chache zenye uwezo wa kuhudumia watoto wenye mahitaji maalum, Serikali imeanzisha mafunzo ya ngazi ya Stashahada (Diploma) katika Chuo cha Ualimu Patandi Arusha na Vyuo vingine ili wahitimu waweze kutoa elimu kwa watoto wenye changamoto ya ugonjwa huo.”amesema Bi.Ziada
Amesema kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kwamba kila vizazi hai 160 wanaozaliwa mmoja hupata tatizo hilo.
Hata hivyo Bi.Ziada amesema ugonjwa wa usonji ni miongoni mwa magonjwa yanayoathiri mfumo wa fahamu wa mtoto ambapo huambatana na kuwa na changamoto kwenye njanya zote za makuzi na mahusiano na watoto wenzake na watu wengine katika jamii.
Amesema dalili za ugonjwa huo huanza kujitokeza katika umri mdogo na mara nyingi kabla mtoto hajatimiza miaka mitatu ambapo amezitaja dalili hizo ni mtoto kushindwa kuongea na kufanya mawasiliano na watu wengine katika jamii,kujitenga na kufanya vitu peke yake, kutoa sauti isiyoashiria kitu.
Aidha amesema watoto wenye ugonjwa huo pia wanaweza kuwa magonja mengine ambatani na miongoni mwa magonjwa hayo ni ,kifafa kuwa na uwezo mdogo wa uelewa na magonjwa mengine ya akili.
“Iwapo wapo wagonjwa wenye usonji na kuwa na kipaji cha hali ya juu kwenye kutambua ama kufanya vitu mbalimbali lakini changamoto za mawasiliano na mahusiano bado zinatawala ugonjwa.
Waziri huyo amesema Serikali inatarajia utoaji wa huduma za utengamao watoto na watu wengine wenye mahitaji maalum ambapo amedai kwa sasa wanaendelea na kuelimisha jamii juu ya uwepo wa tatizo hilo.
“Pia uwepo wa wataalamu wa kutosha kama vile walimu, wataalamu wa huduma kzi kwa vitendo wataalamu wa huduma za mazoezi tiba watoa tiba wa lugha na matamshi pamoja na mtoa tiba wa afya ya jamii na kisaikolojia,”amesema Bi.Ziada
Amesema katika kuadhimisha siku hiyo Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Tamisemi na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia pamoja na Jiji la Dodoma wamedhamiria kuimarisha huduma katika shule ya Mlezi iliyopo Jijini Dodoma.
“Katika awamu ya kwanza tunatarajia vyumba vya madarasa na katika awamu ya pili tunatarajia kuboresha mazingira yaliyopo nje kwa ajili ya kuwapa fursa watoto wetu kuanza kushiriki katika michezo,”amesema Bi.Ziada
Kwa upande wake Afisa Kitengo cha Elimu Maalumu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Bi.Ahiadu Sangoda,amesema kuwa Wizara ya Elimu wataendelea kuboresha huduma na madarasa ya shule za watoto wenye mahitaji maalumu nchini.
”Tutahakikisha tunaimarisha Miundombinu na huduma za watoto wenye uhitaji maalumu lengo likiwa ni kupunguza mzigo wa usonji katika ngazi za kitaifa, kikanda na ndani ya nchi.”amesema
Naye Mstahihi Meya wa Jiji la Dodoma Prof. David Mwamfupe amesema serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalumu.
”Katika mwaka huu wa fedha tayari mkoa wa Dodoma umepokea sh.milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika shule za watoto wenye mahitaji maalumu.”amesema Prof.Mwamfupe
Awali Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili ya Mirembe Dk.Damas Mlaki amesema usonji ni ugonjwa unao wakumba idadi kubwa ya watoto walio kati ya umri wa miaka miwili hadi mitatu na kuathili ukuaji wao.
Dk.Mlaki amesema takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watoto wanaokubwa na tatizo la usonji linaongezeka siku hadi siku.
“Mwaka 2021 tuliwatamua watoto 17 huku idsadi ikizidi kuongezeka kwa mwaka jana ambapo tuliwabaini watoto 48 na kwa mwaka huu katika kipindi cha miezi mitatu tumeshawatambua watoto 26.”amesema
Aidha amefafanua kuwa kutokana na takwimu hizo zinaonyesha kuwa idadi ya watoto wenye usonji imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka hivyo kunahaja ya kuendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha tunakabiliana na tatizo hili.