Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Allan Bukumbi akizungumza na madereva bajaji ambao bajaji zao zimekamatwa kutokana na makosa ya kutotii sheria za barabarani.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Allan Bukumbi akizungumza na madereva bajaji ambao bajaji zao zimekamatwa kutokana na makosa ya kutotii sheria za barabarani.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa Acp Allen bukumbi akionyesha GPS iliyoibwa katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Iringa .
Na Fredy Mgunda, Iringa.
JESHI la Polisi Mkoani Iringa wamekamata bajaji 446 kutokana na sababu mbalimbali huku likiwataka madereva bajaji kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuondokana na ajali zinazohatarisha maisha yao
Amesema kuwa ni vyema vijana hao wakazingatia sheria kwani wamekuwa wakihatarisha maisha yao kutokana na kutotii sheria za barabarani hali ambayo imesababisha moja ya dereva bajaji kupata madhira ya ajali
“katika operesheni hiyo bajaji yenye namba za usajili mc 677 BZL aina ya TVS ilikutwa imetelekezwa katika eneo la kitanzini ndipo walipofika katika eneo hilon na kuikuta bajaji hiyo na kuipeleka katika kituo cha polisi ilipofika majira ya saa sabab mchana askari waliokuwa katika doria maeneo ya samora walipata taarifa kuwa kuna mtu ameonekana mteremko wa kisima cha bibi mlima wa ipogoro ameumia ndipo walipomchukua na kumpeleka hospitalini kijana aliyefahamika kwa jina la Esau Hosea Kilawa ambaye mpaka taarifa za leo asubuhi bado yupo ICU”
Alisema kuwa ni vyema kila mtu akafuata sheria kwani bila hivyo inaweza pelekea jeshi la polisi kudhami dereva bajaji anayekimbia anauhalifu mwingine alioufanya
Katika hatua nyingine Jeshi la polisi mkoani Iringa watu kadhaa kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali ikiwa ni pamoja na manyoya ya mkia wa tembo ,kichwa cha mnayama pundamilia pamoja na nyama ya swala
Hili linakuja baada ya msako wa jeshi la polisi kwa kushirikiana na askari uhifadhi katika msako na hivyo kuwakamata felician modestus mwenye umri wa miaka 46 ,efrahim esiyo mwenye umri wa miaka 51 ,ezekiel remigus umri wa miaka 45 kwa makosa ya kuwa na nayara za serikali .
“Ndugu waandishi wa habari Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa wanyama pori Hifadhi ya Taifa Ruaha tumefanikiwa kuwakamata Efrahim Esiyo ambaye alikutwa na kichwa,mkia na nyama ya pundamilia na silaha moja aina ya gobole,baruti,shoka na panga ndani ya hifadhi ya Ruaha , Ezekiel Remigus mkazi wa kisinga ,Jimale Chilala umri wa miaka 41 mkazi wa nyamakuyu feliecian modestus mponzi mwenye umri wa miaka 46 mkazi wa igangidung’u kwa makosa ya kukamatwa na mfuko wa salfeti wenye manyoya ya tembo”
Aidha ACP Allan Bukumbi alibainisha kuwa wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita kwa kosa la kuwa na mali za wizi
“Tumemkamata fadhili lulandala miaka 31 mkristo fundi simu mkazi wa malingumu amour zahoro miaka 32 muislam mkulima mkazi wa lugalo kelvin mussa miaka 52 mkristo mkulima mkazi wa nyamahanga ,niko nyakunga miaka 40 mkazi wa ilole, baraka mtandi umri wa miaka 36 kutoka malingumu mafinga na ayub sanga miaka 20 mkazi wa ifunda kwa kosa la kuwa na ving’amuzi vinne ,tv tatu aina ya hometech inch 24 redio sub woofer remote mbili za tv simu janja 8 GPS MOJA NA TABLET MOJA”