Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Biashara  Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizitolea ufafanuzi baadhi ya Changamoto za wafanya Biashara katika Jukwaa la kumi na mbili la Biashara la Zanzibar lililofanyika Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Katibu wa  Baraza la Mapinduzi na  Katibu Mkuu Kiongozi ambae pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Biashara (ZNBC) Mhandisi Zena A. Said akitoa taarifa ya utekelezaji wa hoja zilizowasilishwa na Sekta Binafsi katika Mkutano wa tano wa Baraza la Taifa la Biashara la Zanzibar uliofanyika Tarehe 22 Januari,2023,wakati wa  hafla ya jukwaa la kumi na mbili la Biashara la Zanzibar lililofanyika Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.

Mfanya Biashara wa kuuza na kununua Fedha Hassan Ali Nahoda akitoa malalamiko kuhusiana  na upatikanaji wa fedha za kigeni wakati wa  majadiliano katika Jukwaa la kumi na mbili la Biashara la Zanzibar lililofanyika Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais ,Fedha na Mipango Mhe.Sada Mkuya Salum akijibu hoja ya changamoto za upatikanaji wa fedha za kigeni wakati wa  majadiliano katika jukwaa la kumi na mbili la Biashara la Zanzibar lililofanyika Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Mfanya  Biashara wa Kampuni ya Premier Hassan Said Ngozi akitoa changamoto za Bandari kwa Wafanyabiashara wakati wa majadiliano katika Jukwaa la kumi na mbili la Biashara la Zanzibar lililofanyika Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe.Omar Said Shaabani akizungumza wakati alipokua akitoa maelezo mafupi kuhusiana na Jukwaa la Biashara lililofanyika huko Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Washiriki wa jukwaa la kumi na mbili la Biashara la Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ilililofanyika Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.Machi 19,2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.