Wadau mbalimbali waliohudhulia ufunguzi wa Kongamano kubwa la Sauti za Wasichana lililoandaliwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) lililofanyika leo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) Jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja.
Balozi Bw. Paul Sherlock ujumbe wa mshikamano kutoka ubalozi wa Ireland katika ufunguzi wa Kongamano kubwa la Sauti za Wasichana lililoandaliwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) lililofanyika leo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa klabu ya wasichana wa nje ya shule CDF(Kibakwe Mpwapwa), Bi. Grace Mnyanyi akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano kubwa la Sauti za Wasichana lililoandaliwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) lililofanyika leo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) Jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali waliohudhulia ufunguzi wa Kongamano kubwa la Sauti za Wasichana lililoandaliwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) lililofanyika leo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) Jijini Dar es Salaam.
Bi. Caren Shirima amechukua nafasi ya Balozi wa Ireland kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano kubwa la Sauti za Wasichana lililoandaliwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
mwana klabu ya ndani ya shule CDF, Dada Pili Shehe, akiongea na wadau mbalimbali waliojitokeza katika ufunguzi wa Kongamano kubwa la Sauti za Wasichana lililoandaliwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF)kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uswidi lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
*******************************
NA EMMANUEL MBATILO
Wazazi wametakiwa kuwa mstari wa mbele kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike ili kuweza kuwasaidia kufikia Malengo yao.
Hayo yamesemwa leo na wadau mbalimbali katika Kongamano kubwa la Sauti za Wasichana lililoandaliwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uswidi leo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Bi.Lennyster Byalugaba amesema kuwa kongamano hilo litawasaidia wasichana kuweza kukaa kwa pamoja na kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusiana na maisha yao ikiwemo changamoto wanazozipitia kama wasichana.
“Tunategemea kwamba wasichana wenyewe watakaa pamoja na kuandaa mapendekezo ambayo yatawasilishwa kwa mgeni rasmi ambaye atakuwepo kesho kwenye kufunga kongamano ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Tulia Ackson ili aweze kuyafanyia kazi”. Amesema Bi. Lennyster.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa klabu ya wasichana wa nje ya shule CDF(Kibakwe Mpwapwa), Bi. Grace Mnyanyi amesema kuwa Uwepo wa kongamano hilo litawajengea wasichana uwezo wa kujiamini na kufanya na kuonesha uwezo wao walionao katika mambo ya msingi na yenye maendeleo katika jamii.
Naye mwana klabu ya ndani ya shule CDF, Dada Pili Shehe, ameitaka serikali kutunga sheria ambayo itamlinda mtoto wa kike juu ya vitendo vya kikatili vinavyojitokeza katika jamii
“Mtoto wa kike anapaswa kulindwa ili kuweza kufikia malengo yake kwani mtoto wa kike anaweza kuleta mabadiliko katika jamii hivyo wazazi wanatakiwa kuwa kipaumbele kumlinda mtoto wa kike kuepukana na ukatili wa kijinsia”. Amesema Dada Pili.
Kongamano hilo litahusisha majadiliano katika vikundi sita vyenye mada mbalimbali zikiwemo, Wanawake na uongozi, Mifumo ya kisheria na Kisera, Mila kandamizi, Ukatili wa Kingono,Ukatili wa mitandaoni na haki ya afya ya Uzazi.
Hata hivyo kauri mbiu ya Kongamano hilo ni “Binti! Onyesha uwezo wako, leta mabadiliko katika jamii”.