Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati akifunga Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyomalizika leo Machi 18,2023 jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMSEMI, Angellah Kairuki na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary, Semyamule.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ,akisisitiza kwa washiriki wakati akifunga Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyomalizika leo Machi 18,2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki,akizungumza wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,akifunga Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyomalizika leo Machi 18,2023 jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma baada ya kufunga Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyomalizika leo Machi 18, 2023. Wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Kisa Kasongwa baada ya kufunga Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyomalizika leo Machi 18, 2023. Wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Wilaya baada ya kufunga Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyoamalizika leo MACHI 18,2023 jijini Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki na kushoto kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Adolf Ndunguru.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki baada ya kufunga Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyomalizika leo Machi 18,2023 jijini Dodoma. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Wilaya nchini kutatua migogoro iliyopo kwenye maeneo yao na sio kusubiri kiongozi mwingine aje asikilize malalamiko ya wananchi.
Hayo ameyasema leo Machi 18, 2023 jijini Dodoma wakati akifunga Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yaliyofanyika kwa siku sita.
Amesema kuwa wakuu wa wilaya mnatakiwa kwenda kutatua mgogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji ili muweze kuwasaidia wananchi katika masuala hayo.
“Wewe upo hapo unataka Waziri aje aanze kusikiliza kero za mipaka ya vijiji wakati wewe upo,viongozi wa dini wapo,viongozi wa kimila wapo,nenda kasimamie uimarishaji wa mahusiano ya wadau ndani na nje ya nchi,”amesema Mhe.Majaliwa
Aidha amewataka kusimamai utoaji wa huduma za jamii katika maeneo yao kuhakikisheni suala la elimu limetengamaa wanafunzi wanaenda shuleni na madarasa yapo ya kutosha.
“Miundombinu iimarishwe kupitia mapato ya ndani, huduma za afya zitolewe pamoja na kutatua migogoro ya watumishi wa umma na wanachi”amesema
Hata hivyo amewataka kusimamia ajenda za kitaifa ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa ili wananchi wapate huduma inayostahili bila ya kudaiwa au kutoa chochote.
Akizungumzia ruhusa ya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa,Waziri Mkuu amewataka kutumia miongozo iliyopo iliyoainisha juu ya ufanyikaji wa mikutano hiyo.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki , amesema kuwa mafunzo hayo yametolewa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa namna bora ya uongozi,kusimamia rasilimali za fedha na kuwajengea uwezo wa kuwa viongozi wa maamuzi.
“Tunaamini mkirudi katika maeneo yenu ya kazi mtatekeleza yale yote mliyoelekezwa kwa kushirikiana na viongozi wenzenu, watumishi wa umma na wadau na kuepuka migogoro ya kiutendaji katika maeneo yenu ya kazi” ameeleza Mhe.Kairuki