Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akitoa taarifa ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha miaka miwili tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani. Kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Mkoa wa Singida, Yohana Msita na kulia ni Katibu Tawala Msaidizi eneo la Uzalishaji na Uchumi Mkoa wa Singida, Stanslaus Choaji.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKOA wa Singida kwa kipindi cha
miaka miwili ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan tangu awe madarakani
kuanzia 2021/2022 na 2022/2023 bajeti ya
Sekretarieti ya mkoa na Halmashauri imeongezeka kutoka Sh.180,187,060,500 mwaka
2020/2021 hadi Sh.239,808,9771,000 mwaka 2022/2023.
Hayo yameelezwa leo Machi 18, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter
Serukamba wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita
katika kipindi cha miaka miwili tangu Rais Samia aingie
madarakani.
“Ongezeko hili la bajeti limesaidia sana kuboresha huduma za kijamii
na kiuchumi katika mkoa wetu wa Singida” alisema Serukamba.
Alisema mafanikio hayo ya Serikali ya awamu ya sita ni utekelezaji wa ilani
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 20220-2025 na yanapaswa kuungwa mkono na
kila mpenda maendeleo hapa nchini.
Serukamba alisema katika kipindi hicho cha miaka miwili bajeti ya mapato ya
ndani ya Halmashauri imeongezeka kutoka Sh.16,898,296,912 mwaka 2020/ 2021 hadi
kufikia Sh. 22,441,480,865 mwaka 2022/2023.
Aidha, Serukamba aliongeza kuwa
Serikali Kuu imeidhinisha bajeti ya Sh.1,053,240,000 kwa mwaka 2022/
2023 kwa ajili ya kuwalipa madiwaniposho, posho za madaraka kwa watendaji wa
vijiji posho za kila mwezi badala ya fedha hizo kulipwa na halmashauri.
Alisema mpango huo wa Serikali Kuu wa kuwalipa madiwani na watendaji wa
kata na vijiji posho hizo haujawahi kufanyika katika awamu zote za Serikali
zilizopita jambo ambalo limewapa ari ya kufanya kazi kwa bidii watendaji hao.
Akiongelea mafanikio hayo Serukamba alisema mkoa ulipokea Sh.2,850,000,000
kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya utawala katika halmashauri ya Wilaya ya
Singida, Singida Manispaa na Ikungi pamoja na ujenzi wa nyumba za Wakurugenzi
katika Halmashauri za Iramba, Singida na Mkalama.
Serukamba alielezea mafanikio hayo katika sekta mbalimbali zikiwemo za
Afya, Elimu, Uzalishaji, Upatikanaji wa huduma za maji, sekta ya ujenzi,
uchukuzi na mawasiliano, ujenzi wa barabara, ujenzi wa madaraja na Sekta ya
Nishati na Madini alisema Serikali imetoa fedha nyingi katika utekelezaji wa
miradi hiyo.
Serukamba alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Dk. Samia kwa
mafanikio hayo makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka miwili
tangu aingie madarakani na amewaomba watanzania waendelee kumuombea na kuwa
Mungu ampe afya na maisha marefu.
Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro Issa akizungumzakatika mkutano huo kabla ya kumuombea dua Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio makubwaambayo nchi imeyapata katika kipindi cha miaka miwili tangu aingie madarakani.