Mama Janeth Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la mumeweMkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigella akiweka shada ya maua Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Innocent Bashungwa akiweka Shada
Mjumbe wa NEC Zanzibar (vijana) Ndg. Mwanaenzi Hassan Suluhu akiweka shada
***************
Ibada maalumu kuazimisha mwaka wa pili wa kifo chake aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika kanisa la Mt. Yohana Maria Muzeyi Parikoa ya Mlimani, Chato, Geita ikiongozwa na Askofu Mkuu Jimbo la Katoliki la Rulenge, Ngara, Severine Niwemuguzi . Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigella, Mjumbe wa NEC CCM Zanzibar upande wa vijana Ndugu Mwanaenzi Suluhu Hassan na viongozi wengine wa mkoa na wilaya pia walihudhuria.