Kaimu Mkurugenzi Idara ya usalama wa Chakula Wakala wa Chakula na Dawa ZFDA khadija Ali Sheha akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na maghala yasiyo rasmi wakati alipokua akifanya ukaguzi kuangalia usalama na uhalali wa ghala linalomilikiwa na Saleh Hassan khamis huko Mpendae Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Baadhi ya mapolo ya mchele yakiwa katika vifungashio visivyo vya asili katika ghala linalomilikiwa na Saleh Hassan khamis huko Mpendae Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Mmiliki wa ghala lisilorasmi Saleh Hassan khamis akizungumza na waandishi wahabari wakati walipofika katika ukaguzi wa kushtukiza uliofanywa na ZFDA katika ghala hilo liliyopo Mpendae Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi
Baadhi ya maafisa wa Wakala wa Chakula na Dawa ZFDA wakiwa katika ukaguzi kuangalia usalama wa chakula na uhalali wa uwepo wa ghala la Saleh Hassan khamis huko Mpendae Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Kaimu Mkuu wa ukaguzi na uteketezaji ZFDA Eyduu Muhammed Naimu akilifunga ghala linalomilikiwa na Saleh Hassan khamis baada ya kukosa sifa za kuhifadhia Bidhaa,wakati wa ukaguzi uliofanywa na ZFDA kubaini uhalali wa Ghala hilo na usalama wa bidhaa zinazohifadhiwa hapo. .PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.
Na Fauzia Mussa,Maelezo
Wakala wa chakula na dawa Zanzibar ZFDA wameifungia ghala iliyokua ikihifadhi bidhaa mbalimbali ikiwemo mchele kutokana na ghala hiyo kukosa sifa za kuhifadhia bidhaa hizo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa kushtukiza kuangalia usalama wa chakula,na uhalali wa uwepo wa ghala hilo huko Mpendae Kaimu Mkurugenzi Idara ya usalama wa chakula ZFDA khadija Ali Sheha amesema ukaguzi umebaini kuwa ghala hilo halijasajiliwa,haliko katika hali ya usafi na haliruhusu hewa kupita hali inayopelekea chakula kinachihifadhiwa hapo kutokua salama.
Alisema kuwa usalama wa chakula ni jukumu la Kila mmoja hivyo ameitaka jamii kutoa taarifa mapema mara tu wanapoona Hali isiyokuwa ya kawaida katika maghala ya kuhifadhia chakula
“Kwapamoja sasa tushirikiane kulinda Afya zetu kwa kuyafichuwa maghala kama haya ambayo yanahatarisha Afya za watu na kuitia hasara Serikali” alishauri kaimu huyo.
Aidha katika ukaguzi huo ZFDA wamebaini Kua mmiliki wa ghala hilo amekua akiziba vifungashio vya asili Kwa baadhi ya bidhaa zilozuiliwa kusafirishwa nje ya Zanzibar ikiwemo mchele aina ya mapembe katika maboksi na vipolo ili kurahisisha usafirishaji Jambo ambalo ni kosa kisheria.
Kwa upande wake mmiliki wa ghala hilo Saleh Hassan Khamis amesema kuwa amekua akizifunga tena bidhaa hizo katika mapolo na maboksi ili kuzihifadhi na kuziweka salama wanapokua safarini bila kufahamu kufanya hivyo kama ni kosa kisheria, hivyo saleh ameiomba ZFDA kuwapatia elimu Wafanyabiashara ili kuepuka makosa yasiyotarajiwa.
Nae Sheha wa Shehia ya Mpendae suleiman Ali Makuu amewasihi wafanya Biashara kuwa waaminifu na kuwataka wafuate Sheria zilizowekwa na Serikali ili kuepuka matatizo wakati wanapofanya Biashara zao.
Katika Ukaguzi huo mbali na bidhaa nyengine jumla ya polo mia tatu za mchele aina ya mapembe yenye ujazo wa kilo hamsini yamekutikana katika ghala hilo ambalo halijasajiliwa.