NAIBU Katibu mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Franklin Rwezimula,akizungumza wakati akifungua kongamano la kujadili namna ya kupata vyanzo vipya vya mapato vitakavyo tumika kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB) lililofanyika leo Machi 16,2023 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)Prof. Hamis Dihenga ,akizungumza wakati wa kongamano la kujadili namna ya kupata vyanzo vipya vya mapato vitakavyo tumika kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB) lililofanyika leo Machi 16,2023 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Bodi ya mikopo wanafunzi wa elimu ya juu Zanzibar (ZHELB) Prof.Mohammed Hafidh Khalifa,akizungumza wakati wa kongamano la kujadili namna ya kupata vyanzo vipya vya mapato vitakavyo tumika kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB) lililofanyika leo Machi 16,2023 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa kongamano la kujadili namna ya kupata vyanzo vipya vya mapato vitakavyo tumika kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB) lililofanyika leo Machi 16,2023 jijini Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul- Razaq Badru ,akizungumza wakati wa kongamano la kujadili namna ya kupata vyanzo vipya vya mapato vitakavyo tumika kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB) lililofanyika leo Machi 16,2023 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Franklin Rwezimula,akiwa katika picha na washiriki mara baada ya kufungua kongamano la kujadili namna ya kupata vyanzo vipya vya mapato vitakavyo tumika kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB) lililofanyika leo Machi 16,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI kwa kushirikiana na wadau wa Sekta ya Elimu imeanza mkakati wa kutafuta vyanzo vipya vya mapato ambavyo ni endelevu ili kuwezesha wanafunzi wote wanaostahili kupata mkopo waweze kupata na kujiunga na masomo ya elimu ya juu (HESLB).
Hatua hiyo inafuatia baada ya mageuzi makubwa yaliyofanywa na serikali katika sekta ya elimu na hivyo kupelekea uwepo wa ongezeko la wanafunzi wanaohitimu masomo na kuhitaji kujiunga na elimu ya juu.
Hayo yamesemwa leo Machi 16,2023 jijini Dodoma na Naibu Katibu mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Franklin Rwezimula,wakati akifungua kongamano la kujadili namna ya kupata vyanzo vipya vya mapato vitakavyo tumika kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB)
Dkt. Rwezimula amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ipo katika mageuzi makubwa ya elimu ambayo yataongeza fursa kwa vijana wengi kujiunga na elimu ya juu na hivyo kuongeza uhitaji wa fedha kwa ajili ya kugharamia masomo hayo.
“ Sasa hivi tunaitegemea Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) pekee yake, ambayo hivi sasa haikidhi mahitaji hivyo tumeamua kukutana na wadau kutoka sekta mbalimbali ili kujadili kwa pamoja na kupata vyanzo vipya ambavyo vitasaidia kusomesha watoto wetu wasiokuwa na uwezo”amesema Dk.Rwezimula
Aidha Dk.Rwezimula amesema Kongamano hilo litajadili namna bora ya kupata vyanzo hivyo vipya na kuja na maadhimio ambayo yatatoa mwelekeo wa kupata fedha ambazo zitatumika kuhudumia wenye uhitaji.
“Sasa hivi tumepata benki ya NMB, ambao tayari wametenga Sh. bilioni 200 ambapo watu wataweza kukopo kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu na riba yao ni asilimia tisa, kwahiyo bado tunahitaji kupata wadau wengine watakaohudumia watoto wengi katika vyuo vyetu”ameeleza Dk.Rwezimula
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Prof. Hamis Dihenga amesema kongamano hilo linalenga kuhakikisha wanajadili na kutathimin njia mbalimbali zitakazowezesha ugharamiaji wa elimu ya juu unakuwa na vyanzo vingi na endelevu badala ya kusubiri fungu kutoka serikalini pekee.
“Lengo letu kupitia mkutano huu ni kupata vyanzo vipya vya mapato hatuwezi kuendelea kutegemea serikali pekee yake kwakua ina mambo mengi bado zipo changamoto nyingi na idadi ya wanafunzi wenye sifa ya kupata mikopo inaongezeka kila mwaka hivyo ni lazima tujadiliane ili kutoka na majibu ya kuwa na vyanzo vipya vya mapato”amesema Prof.Dihenga
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya mikopo wanafunzi wa elimu ya juu Zanzibar (ZHELB) Prof.Mohammed Hafidh Khalifa,amesema kuwa hivi sasa kuna watoto wengi nchini ambao wanahitaji kupata mikopo lakini vyanzo vinavyotegemewa ni Bodi za mikopo ya elimu ya juu za Zanzibar na Tanzania bara.
“Mkutano wetu huu leo utatusaidi kupata namna bora ya kupata vyanzo vipya vya mapato ili kila mtoto anayestahili kujiunga na masomo ya elimu ya juu ajiunge bila kuwapo na kikwazo chochote”amesema Prof. Khalifa
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Abdul- Razaq Badru amesema Bodi hiyo inatekeleza mageuzi makubwa ya kimfumo ya usimamizi, uendeshaji pamoja na shughuli ambazo bodi inasimamia.
“Tathimini ya kwanza ni kuangali sisi kama serikali wale tunao walipita kusoma shahada wanazozisoma kama zinaendana na soko la ajira, tathimini nyingine ni kuangalia namna gani ya kupata vyanzo vipya kwa ajili ya kulipia watoto kwa mwaka huu tuu serikali imetoa Sh. bilioni 654 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi elimu ya juu”amesema Bw.Badru