Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya Elimu Dk. Charles Msonde akizugumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Machi 15,2023 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa wanafunzi wa Kidato cha nne kufantya mabadiliko ya Tahasusi.
Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imetoa muda wa wiki tatu kwa wahitimu wote wa kidato cha nne kwa mwaka 2022/23 kufanya mabadiliko au maboresho ya tahasusi walizokuwa wamechagua awali lengo likiwa kuwawezesha kufanya machaguo sahihi kulingana na ufaulu binafsi wa Mwanafunzi.
Kauli hiyo imetolewa leo Machi 15,2023 jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya Elimu Dk. Charles Msonde wakati akizugumza na waandishi wa habari,
Dk.Msonde amesema kuwa siku 21 itamuwezesha mwanafunzi kurekebisha machaguo yake kulingana na ufaulu wake alioupata kwenye mataokeo ya mtihani wa kumaliza kidato cha nne 2022.
Aidha amesema kuwa machaguo haya yamekuwa yakifanyika shuleni kabla ya wanafunzi hao kuhitimu lakini matokeo yakitoka baadhi wamekua walikosa sifa ya kuchaguliwa.
”Utaratibu wa wanafunzi kubadilisha machaguo yao unaanza leo Machi 15,2023 hadi April 6,2023 hivyo nawaomba wazingatie muda uliotolewa wa kufanya marekebisho hayo ili ratiba ya kuwachagua na kuwapangia shule na vyuo iweze kuendelea kwa muda uliopangwa”amesema Dk.Msonde
Hata hivyo Dk.Msonde amewataka wazazi na walezi kushiriki katika zoezi hilo kwa kushaurina na mtoto katika machaguo yake kulingana na ufaulu ili kuepukana na adha ya wanafunzi wengi kuchagua shule moja hivyo kupelekea kosa nafasi.
”Tafadhali mzazi kubaliana na mtoto katika machaguo yake ili baada ya zoezi la uchaguzi pasiwepo malalamiko yoyote ya kwamba mtoto amepangiwa machaguo ambayo hakuyachagua”amesisitiza Dk.Msonde
Uchambuzi wa matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne (CSEE) Mwaka 2022 watahiniwa 456, 975 sawa na asilimia 87.79 waliopata alama ya kwanza hadi ya tatu ni watahiniwa 192,348 ndio waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano sawa na asilimia 36.95