Na.Elimu ya Afya kwa Umma.
Jumla ya washiriki 107 wameshiriki katika maadhimisho ya siku ya Afya na Lishe Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera ambapo
katika maadhimisho hayo mwitikio wa wanaume umekuwa mkubwa .
Pichani ni Matukio mbalimbali katika Maadhimisho ya siku ya Afya na Lishe Wilaya ya Karagwe ,jumla ya washiriki 107 wameshiriki, .
Hata hivyo, Wilaya ya Meatu Meatu Mkoani Simiyu nayo haikuachwa nyuma katika maadhimisho hayo ambapo Afisa lishe katika wilaya hiyo Anna Msangi kwa kushirikiana na watoa huduma wametumia fursa ya maadhimisho hayo kutoa elimu ya afya kuhusu lishe, umuhimu wa chanjo ya HPV kwa watoto na kuhamasisha chanjo kwa watoto walioacha mtiririko wa chanjo huku wanafunzi 10 Shule ya Msingi Isingiro Wilaya Kyerwa Mkoa Kagera nao pia wakipata chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi (HPV)
Afisa Lishe Wilaya ya Meatu pamoja na watoa huduma wakitoa elimu ya Afya kuhusu lishe, umuhimu wa chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi(HPV )kwa watoto na kuhamasisha chanjo kwa watoto walioasi chanjo leo Tarehe 13/3/23 katika hospital ya Wilaya ya Meatu
Wanafunzi 10 wa Shule ya msingi Isingiro Wilaya Kyerwa Mkoa Kagera waliopata chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi (HPV)
Ikumbukwe kuwa siku ya Maadhimisho ya Afya na Lishe huadhimishwa kwa lengo la kuikumbusha jamii umuhimu wa kuzingatia kanuni bora za Afya ikiwemo kuzingatia lishe bora ili kuepukana na udumavu, unene uliopitiliza, na umuhimu wa kufanya mazoezi.