Afisa mwana sheria wa Baraza la Ushindani halali wa Biashara Zanzibar (ZFCT) Mgeni Abdulla Mohammed akitoa maelezo kuhusiana na Baraza hilo wakati alipotembelewa na Waandishi wa Habari huko Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge,ikiwa ni shamrashamra za kuadhimishi wiki ya kumlinda mtumiaji, na kufikiwa kilele chake tarehe 15 mwezi huu Jijini Mwanza yakiwa na kauli mbiu “kumjengea uwezo mtumiaji katika matumizi ya nishati na nishati mbadala” .PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR. 14.03.2023
Afisa uhusiano Tume ya Ushindani halali wa Biashara Zanzibar (ZFCC) Ibrahim Hamad Makame akiwaonyesha Waandishi wa Habari mfano wa Bidhaa iliyokopiwa wakati alipokua akiwapatia elimu kuhusiana na haki za mtumiaji katika shamrashamra za wiki ya kumlinda mtumiaji zilizofanyika Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge ,na kufikiwa kilele chake tarehe 15 mwezi huu Jijini Mwanza yakiwa na kauli mbiu “kumjengea uwezo mtumiaji katika matumizi ya nishati na nishati mbadala” .PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR. 14.03.2023
***************************
Na Rahma Khamis,Maelezo
Wananchi wametakiwa kuchukua risiti zao wakati wanapokwenda kupeleka malalamiko katika baraza la Ushindani Halali wa Biashara Zanzibar (ZFCT) ili kuepuka usumbufu wakati wa kutatuliwa malalamiko yao .
Wito huo umetolewa na Afisa Mwanasheria wa hilo Mgeni Abdulla Mohammed katika Uwanja wa Mnara wa kumbukumbu Kisonge wakati alipokua Akitoa elimu kwa wananchi kuhusu haki ya mtumiaji katika bidhaa ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya kumlinda mtumiaji.
Amesema risiti ni jambo muhimu kwa mlalamikaji kutokana na kuwa ni ushahidi tosha utakaomuongoza mtoa maamuzi katika kulitafutiwa ufumbuzi lalamiko alilofikishiwa na mtumiaji.
Aidha Mwanasheria amesema kila mtu ni mtumiaji wa bidhaa katika jamii hivyo ni wajibu wao kufahamu haki na wajibu wao ili kuepuka matatatizo yanayoweza kujitokeza.
“Watu wote ni watumiaji kama hatujatumia Mchele tunanunua bidhaa nyengne au tunapanda usafiri hivyo ni wajibu wetu kujua haki zetu katika kutumia bidhaa ili malalamiko yanayoweza kuepukika .” alisema Mwanasheria.
Hata hivyo Mwanasheria huyo amewasisitiza wananchi kuangalia bidha zao wanaponunua kabla ya matumizi ili kuepusha madhara yanayoweza kujitikeza .
Nae Afisa Uhusiano wa Tume ya Ushindani Halali wa Biashara Ibrahim Hamad Makame amesema mtumiaji ana haki ya kulindwa dhidi ya bidhaa na huduma zisizo salama ambazo zinaweza kuangamiza Mali na kuhatarisha Afya ya mtumiaji.
Aidha amefahamisha kuwa mbali na kutambua haki yake pia ana haki ya kupata maelezo sahihi kuhusu bei,ujazo na malighafi zinazounda bidhaa zitakazomuezesha kufanya maamuzi ya kununua bidhaa sahihi.
Kwa upande wao wananchi wamesema kuwa wamefarajika kupatiwa elimu hiyo kwani walikua hawfahamu chochote kuhusu haki za mtumiaji wa bidhaa.
Kilele cha Maashimisho ya wiki ya kumlinda mtumiaji yanatarajiwa kufanyika kesho Jijini Mwanza ambapo Kaulimbiu ya mwaka huu “KUMJENGEA UWEZO MTUMIAJI KATIKA MSTUMIZI YA NISHATI NANISHATI MBADALA.”