Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfano wa barabara yenye alama muhimu za usalama barabarani katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, Machi 14, 2023. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya, kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima na wa tano kulia ni Kamishina Jenerali wa Jeshi la Polisi, Camilius Wambura. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM, Sixbert Reuben na kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Jamal Babu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza ambako alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama kwenye viwanja vya Furahisha.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati akizindua Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteremka kutoka kwenye basi baada ya kulikagua akiwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, Machi 14, 2023. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkaguzi wa Polisi, Dumu Mwalugege (kulia) ambaye alitoa maelezo kuhusu alama za usalama barabarani katika maonyesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalam Barabarani yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Furahish jijini Mwanza, Machi 14, 2023. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima na wa pili kushoto ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Camilius Wambura.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza,
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)