Kiongozi wa Msafara wa Watumishi Wanawake wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Bi.Sylvia Lupembe,akimkabidhi Keki Mkuu wa Shule Kigwe Viziwi Thadei Mhwagila kwa ajili Kukata Keki hiyo pamoja na kusherekea na wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Kiongozi wa Msafara wa Watumishi Wanawake wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Bi.Sylvia Lupembe,akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kigwe Viziwi iliyopo wilayani Bahi Mkoani Dodoma wakati wa kusherekea siku ya wanawake duniani kwa kukata keki,kupanda miti na kutoa misaada ya vifaa mbalimbali.
WATUMISHI Wanawake Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,wakifurahi pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kigwe Viziwi wakati wakikata keki katika kusheherekea siku ya wanawake Duniani.
WATUMISHI Wanawake Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,wakigawa Keki pamoja na Juice kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kigwe Viziwi wakati wa kusheherekea siku ya wanawake Duniani.
WATUMISHI Wanawake Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, wakikabidhi Vifaa mbalimbali kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kigwe Viziwi ambapo wamesheherekea siku ya wanawake duniani kwa kukata keki,kupanda miti na kuwapatia mahitaji muhimu wanafunzi hao.
Kiongozi wa Msafara wa Watumishi Wanawake wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Bi.Sylvia Lupembe,akiwa na Wanawake Wizara ya Elimu ,Mkuu wa Shule na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kigwe Viziwi wakipanda mti katika shule hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Kiongozi wa Msafara wa Watumishi Wanawake wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Bi.Sylvia Lupembe,akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali pamoja na kukata keki,Kupanda Miti katika Shule ya Msingi Kigwe Viziwi iliyopo wilayani Bahi Mkoani Dodoma wakati wa kusherekea siku ya wanawake Duniani .
Mkuu wa Shule Kigwe Viziwi Thadei Mhwagila,akitoa pongeza kwa Watumishi Wanawake wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,kwa kwenda kuwafariji Wanafunzi wake kwa kula Keki pamoja na kugawa Misaada ya vifaa mbalimbali wakati wa kusherekea siku ya wanawake Duniani .
WATUMISHI Wanawake wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kigwe Viziwi wakati wakisheherekea siku ya wanawake duniani ambapo wamekata keki,kupanda miti na kuwapatia mahitaji muhimu wanafunzi hao.
Na.Alex Sonna-BAHI
WATUMISHI Wanawake wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, wamesheherekea siku ya wanawake duniani kwa kukata keki,kupanda miti na kuwapatia mahitaji muhimu wanafunzi wa shule ya msingi Kigwe Viziwi wilayani Bahi mkoani Dodoma.
Akizungumza kwa niaba ya wanawake hao, katika shule hiyo, Sylvia Lupembe,amesema katika kusheherekea siku ya wanawake Duniani Watumishi Wanawake wa Wizara hiyo wameamua kusheherekea na wanafunzi hao kwa kukata keki pamoja nao.
Amesema kuwa pamoja na kukata keki wamekabidhi vifaa mbalimbali katika shule hiyo ambavyo ni Simtank lita 4000, Mashuka, Mipira ,Taulo za kike,Magodoro, Juice, Biscuit ,keki
“Tumekuja kama wazazi,walezi na wenzao kwa sababu ni eneo letu la kisera,tumekuja kuwaona na kuwatia moyo kwamba wanaweza na wapo shule wanaweza,”amesema Lupembe.
Amesema Wizara inasaidia kwa kuwekeza kiasi kikubwa kuhakikisha kuna kuwa na miundombinu rafiki ya wao kuweza kupata elimu.
“Leo tumekuja na mahitaji ambayo waliyataja wao wenyewe tumewaletea magodoro ambayo yatawafanya walale kwenye mazingira rafiki lakini tumewaletea mashuka na Matanki ya maji pamoja na taulo za kike kwa watoto wa kike,”amesema Lupembe
Amesema kwa sababu wapo katika msimu wa sherehe wameenda kufurahi pamoja na kula keki na wamepanda miti kwa pamoja na wanafunzi hao.
“Mwaka huu wanawake tunasheherekea kwa kudhamini ubunifu teknolojia na sisi tumesikia kutoka kwao kwamba wanahitaji vifaa vya tehama vikiwemo Vishkwambi eneo hili tunaliona ni la kimkakati tunatakiwa kulifanyia kazi,”amesema Lupembe.
Amesema wanafurahi kuona wanafunzi hao wanafundishwa malezi na stadi za maisha ambazo zitakuja kuwasaidia katika maisha yao.
“Sisi kama Wanawake tunasema tumetumia nguvu zetu na kidogo tulichokipata kula na kufurahi na watoto wetu,”amesema Lupembe.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule Kigwe Viziwi Thadei Mhwagila amesema wanashukuru watumishi wanwake wa wizara ya Elimu kwa ugeni huo kwani wanafunzi wamefurahi.
Amesema Watumishi Wanawake whao wamewajengea upendo ambao wanahisi walikuwa wanaukosa katika maeneo wanayoishi.
“Tunapenda kushukuru kwa hicho wametoa msaada mkubwa kwa sababu watoto hawa wanaishi na Bibi zao mara nyingi wanakosa mahitaji ya msingi,”amesema Mhwagila
Hata hivyo ametoa ushauri kwa wazazi na walezi kuwaona watoto wote wapo sawa na kuwathamini watoto hao.
“Nitoe shukrani kwa Serikali kwa kuwajali hawa watoto wametuletea fedha kujenga mabweni wataishi katika mazingira mazuri,”amesema Mhwagila
Naye,Afisa Elimu,Elimu Maalum,Idara ya Elimu Msingi,Wilaya ya Bahi,Sarah Chizingwa amewashukuru Wanawake wa Wizara ya hiyo kwa kutoa misaada hiyo na kuwaona watoto hao.
“Tunafurahi kwa upendo mliotuonesha sisi kwa kuja kuwaona wototo wetu wenye ulemavu ambao ni viziwi tumepokea zawadi zenu na Mungu awabariki pale mlipuoungukiwa Mungu awaongezee tunawakaribisha wakati mwingine Bahi,”amesema Chizingwa