Mwenyekiti kamati za wanawake TUGHE mkoa wa Arusha,Tatu Furahisha akikabithi misaada hiyo kwa uongozi wa hospitali ya ALMC iliyopo jijini Arusha.
Katibu wa TUGHE mkoa wa Arusha ,John Mahimbo akizungumza katika hospitali hiyo wakati wakifanya usafi .
Julieth Laizer,Arusha.
Arusha.Chama cha wafanyakazi wa serikali na Afya Tanzania (TUGHE) mkoani Arusha wamekabithi misaada mbalimbali katika hospitali ya ALMC kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa mbalimbali waliolazwa katika hospitali hiyo.
Aidha misaada iliyokabithiwa ni pamoja na mashuka 22, Pampers,pamoja na sabuni ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika hospitali hiyo.
Akizungumza wakati wa kukabithi misaada hiyo ,Mwenyekiti wa kamati za wanawake TUGHE mkoa wa Arusha,Tatu Furahisha amesema kuwa,wamefikia hatua ya kufanya matendo ya huruma kwa hospitali hiyo ikiwa ni mwendelezo wa siku ya wanawake duniani katika kushirikiana nao kile kidogo walichojaliwa.
Tatu amesema kuwa,kama chama ni utamaduni wao kuhakikisha wanasaidia kupitia kile kidogo wanachokipata ambapo wamekuwa wakisaidia watoto waishio kwenye mazingira magumu,wajane pamoja na kuwalipia ada watoto wasiojiweza na kuangalia mahali penye uhitaji na kuweza kupeleka misaada mbalimbali.
“nitoe wito kwa vyama vingine pia kufanya matendo ya huruma kwa kuwasaidia watu wenye uhitaji katika kuondokana na changamoto mbalimbali kwa kurudisha kile kidogo wanachopata kwa jamii ili nao wanufaike na uwepo wa vyama hivyo. “amesema Tatu.
Aidha ametoa wito kwa wafanyakazi ambao hawajajiunga na TUGHE kujiunga na chama hicho ili waweze kuwa kitu kimoja na kuweza kutetea maslahi ya wafanyakazi kwa pamoja .”amesema.
Kwa upande wake Katibu wa TUGHE mkoa wa Arusha ,John Mahimbo amesema kuwa,umekuwa ni utaratibu wao kusaidia jamii kila mwaka ambapo wamekuwa wakifanya matendo ya huruma kwa jamii katika hospitali mbalimbali ambapo kwa mwakani wataenda hospitali nyingine.
Mahimbo amesema kuwa,wanachokifanya wake ni kurudisha kwa jamii kile kidogo wanachopata ambapo amewataka wengine kuiga mfano kama huo kusaidia jamii kuondokana na changamoto mbalimbali.
Aidha kwa pamoja wameshukuru TUGHE makao makuu na uongozi wa mkoa pamoja na kamati ya wanawake ya mkoa katika kuwezesha fedha na uratibu wa shughuli hiyo .
Mwenyekiti wa wanawake tawi la ALMC ,Magdalena Shangay ameshukuru chama hicho kwa kuwasaidia misaada hiyo ili wapate ahueni wakati wakiendelea na matibabu zaidi huku akivitaka vyama vingine kusaidia jamii inayowazunguka kama walivyofanya chama hicho.