Askari wa Jeshi la Polisi kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) wamewafariji mahabusu na wafungwa katika Gereza la Segerea lengo likiwa ni kutambua kundi hilo muhimu kwa taifa.
Akiongea na waandishi wahabari mwenyekiti wa mtaandao wa Polisi wanawake kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam mrakibu mwandamizi waw a Polisi SSP-ANITHA SEMWANO amesema wanatambua umuhimu wa kundi hilo katika jamii ambapo amesema wao kama Jeshi la Polisi walitumia siku ya wanawake duniani kuwapa elimu ya ukalii wa kijinsia na namna ya kutoa taarifa za ukalii katika jamii.
Aidha SSP Mwano amesema kundi hilo lipo katika gereza hilo kwa mujibu wa sheria na kusema kwamba wao walikinzana na sheria za Nchi la Jeshi hilo linatambua mchango mkubwa Kubdi hilo ambapo amebainisha kuwa wakufunzi wa chuo hicho Pamoja na wanafunzi wa kozi ya uofisa na mkaguzi msaidizi wa Polisi waliona vyema kuungana na kutoa mchango huo kwa wafungwa waliopo katika gereza hilo.
Nae mrakibu wa Magereza SP IYUNGE SAGANDA amesema mchango wa askari hao utakuwa msaada mkubwa kwa wafungwa hususani wafungwa kike ambapo ametoa wito majeshi na taasisi nyingine kuiga mfano mzuri wa Jeshi la Polisi kwa kumbuka makundi ya wahitaji.
Sambamba na hilo mwanafunzi wa kozi ya mkaguzi msadizi wa Polisi WP GIFT MSOWOYA amesema wao wanatambua umuhimu wa kundi hilo mara watakapomaliza kifungo chao ambapo amesema wanamchango mkubwa katika ujenzi wa taifa.
Kwa upande kwa mkuu wa chuo cha taaluma ya Polisi Dar es salaam ambae ndiye mlezi wa mtaandao huo kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Daktari Lazaro Mambosasa amewapongeza askari hao kwa moyo wao wa kipeke wa kujali makundi maaalum.