Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa kutoa Kiasi cha Shilingi Bilioni 90 za ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Lami kuanzia Kibada kuzunguka Mwasonga na Kisarawe Two ikiwa nisehemu ya kutatua kero za ubovu wa barabara kwa wananchi wa Wilaya hiyo.
RC Makonda ameeleza hayo leo wakati wa Ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya maendeleo Wilaya ya Kigamboni na kueleza kuwa Serikali imedhamiria kufanya mji wa Kigamboni kuwa wa kisasa hivyo amewahimiza wananchi kuhakikisha wanaepuka ujenzi holela, uuzaji wa viwanja bila taratibu pamoja na Ujenzi bila Vibali.
Katika ziara hiyo RC Makonda ametembelea ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni lenye thamani ya Shilingi Billion 5.3 ambapo amewataka TBA kuhakikisha wanakamilisha jengo hilo kabla ya Disemba 30 na kubainisha kuwa jengo hilo ndio jengo kubwa kuliko majengo yote ya halamshauri Nchini.
Aidha RC Makonda ametembelea ujenzi wa Majengo 7 ya Hospital ya Wilaya ya Kigamboni ambayo ujenzi wake umekamilika na kugharimu kiasi cha shilingi Billion 1.5 kupongeza Manispaa hiyo kwa kukamilisha ujenzi huo mapema.
TUKUTANE SITE 2019.