Wanawake watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida wakionesha furaha yao kabla ya kwenda kupanda miti kwenye chanzo cha maji cha Mwankoko kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Singida ikiwa ni shamra shamra kuelekea
kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, kesho Machi 08,2023.
Na Dotto Mwaibale, Singida
WANAWAKE watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) na wenzao wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani Machi 08, 2023, wamepanda miti katika chanzo za maji cha Mwankoko kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya
Singida ikiwa ni moja ya kazi ya upandaji miti ili kuimarisha uoto wa asili
utakaosaidia upatikanaji wa mvua na hivyo kuimarisha vyanzo vya maji kwa ajili
ya kuzalisha umeme mwingi.
(TANESCO) na wenzao wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani Machi 08, 2023, wamepanda miti katika chanzo za maji cha Mwankoko kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya
Singida ikiwa ni moja ya kazi ya upandaji miti ili kuimarisha uoto wa asili
utakaosaidia upatikanaji wa mvua na hivyo kuimarisha vyanzo vya maji kwa ajili
ya kuzalisha umeme mwingi.
Mbali na upandaji miti wanawake hao wa TANESCO wametoa
msaada wa unga, mafuta ya kula, sabuni na vitu vingine kwa watoto yatima wa Kituo cha Upendo Home for Street Children, ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku hiyo
ambayo duniani kote yatafanyika kesho.
msaada wa unga, mafuta ya kula, sabuni na vitu vingine kwa watoto yatima wa Kituo cha Upendo Home for Street Children, ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku hiyo
ambayo duniani kote yatafanyika kesho.
Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika leo
Machi 7, 2023 kwa kuwashirikisha wakuu wa idara wa taasisi hizo mbili za
Serikali mkoani hapa.
Akizungumza katika zoezi hilo la
upandaji miti Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo, Lulu Silungwe alisema TANESCO imekuwa
ikitegemea mvua inayotokana na miti kwa ajili ya kusambaza huduma ya umeme
hivyo zoezi hilo la upandaji wa miti litasaidia kukabiliana na athari za
kimazingira na mvua kuwa nyingi.
“Tumekutana hapa leo na wenzetu kutoka SUWASA kwa ajili ya kupanda miti chanzo cha maji Mwankoko chini ya kauli mbiyu
yetu isemayo Panda Miti, Mvua Ndi, Umeme Ndindindi ikiwa ni moja ya kazi yetu
kuelekea maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani ambayo ni kesho”
alisema Silungwe.
Alisema mbali ya kupanda miti pia
watawatembelea watoto Yatima wanaolelewa Kituo cha Upendo Home for Street
Children, kwa ajili ya kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwa ni kazi yao nyingine
kuelekea maadhimisho hayo.
Neema Ntandu ambaye ni mfanyakazi wa
shirika hilo alisema wamepanda miti 150 ya aina mbalimbali na kuwa
watahakikisha inakuwa na kuimarisha chanzo hicho cha maji cha Mwankoko.
Mwenyekiti wa Wanawake wa Shirika hilo
Mkoa wa Singida, Asiatu Mnanura akizungumza wakati wa kutoa msaada kwa watoto wa
kituo hicho alisema wamefurahi kuwatembelea ukizingatia kuwa wao ni wazazi
hivyo waliona vizuri jambo hilo liwe ni sehemu ya moja ya kazi yao kuelekea
maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala
wa SUWASA, Fatina Mbaga alisema ni wajibu kwa kila mwana Singida kupanda miti
kwa wingi ili kuhifadhi mazingira jambo litakalosaidi kuhifadhi mazingira na kuwepo
kwa mvua nyingi na hivyo kuwa na maji ya kutosha.
Mratibu wa kituo hicho Afesso Ogenga alishukuru
kwa msaada huo na kueleza kuwa kituo hicho kinawapokea watoto kutoka mitaani na
majumbani lakini ni baada ya kufanyika utaratibu wa kuwatambua na kujua
historia zao kwa kushirikiana na watu wa ustawi wa jamii.
Wanawake watumishi wa Tanesco Mkoa wa Singida wakifanya maandamano kuelekea katika zoezi hilo la kupanda miti.
Mratibu wa Kituo cha Home for Street Children, Afesso Ogenga akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada huo.
Wanawake watumishi wa Suwasa Mkoa wa Singida wakipanda ngazi kuingia kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda kupanda miti.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Suwasa, Fatina Mbaga, akizungumzia kuhusu zoezi hilo la upandaji miti.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Suwasa, Fatina Mbaga, akipanda mche wa mti.
Neema Ntandu ambaye ni mfanyakazi wa shirika hilo, akizungumzia umuhimu wa kupanda miti katika vyanzo vya maji.