Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Yusuph Hassan Iddi wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Udhibiti Ubora TBS, Bw.Gervas Kaisi namna Ofisi ya TBS bandarini inavyofanya shughuli zake mara baada ya Kamati hiyo kutembelea Ofisi hiyo leo Machi 7,2023 Jijini Dar es Salaam Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Yusuph Hassan Iddi wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Udhibiti Ubora TBS, Bw.Gervas Kaisi namna Ofisi ya TBS bandarini inavyofanya shughuli zake mara baada ya Kamati hiyo kutembelea Ofisi hiyo leo Machi 7,2023 Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar Mhe. Yusuph Hassan Iddi akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya mara baada ya Kamati hiyo kufanya ziara katika Ofisi za TBS bandarini leo Machi 7,2023 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Zanzibar Mhe.Omar Shaaban akizungumza jambo na Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe katika ziara ya Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar \kutembelea Ofisi za TBS bandarini leo Machi 7,2023 Jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Bodi TBS, Prof.Athuman Chande (kulia) akiwa pamoja Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya wakimsikiliza Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe mara baada ya Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar kufanya ziara katika Ofisi za TBS bandarini leo Machi 7,2023 Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar Mhe. Yusuph Hassan Iddi akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati hiyo, pamoja na Watumishi wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) mara baada ya Kamati hiyo kufanya ziara katika Ofisi za TBS bandarini leo Machi 7,2023 Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akizungumza mbele ya Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar mara baada ya Kamati hiyo kufanya ziara katika Ofisi za TBS bandarini leo Machi 7,2023 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya akizungumza mbele ya Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar mara baada ya Kamati hiyo kufanya ziara katika Ofisi za TBS bandarini leo Machi 7,2023 Jijini Dar es Salaam.
Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Yusuph Hassan Iddi wakiwa katika Maabara za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) baada ya kutembelea Ofisi za Makao Makuu ya TBS leo Machi 7,2023 Kujiona na kujifunza kupitia shughuli ambazo zinafanywa na Shirika hilo.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*******************
Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar imeipongeza Shirika la Viwango Tanzania kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake katika kuhakikisha inaandaa viwango stahiki kwa bidhaa zinazozalishwa nchini na zinazoingia kutoka nje ya nchi ili kumlinda mlaji ama mtumiaji.
Pongezi hizo zimetolewa leo Machi 7,2023 mara baada ya Kamati hiyo kufanya ziara katika ofisi za TBS bandarini pamoja na TBS Makao Makuu Jijini Dar es Salaam ili Kujifunza Shughuli ambazo zinafanywa na Taasisi hiyo.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar Mhe. Yusuph Hassan Iddi amesema wameweza kujifunza masuala mengi yanayofanywa na TBS hasa kwenye ofisi zao zilizopo bandarini pamoja na mifumo ambayo wameunganisha ili kurahisisha masuala mazima ya ukaguzi na utoaji mizigo bandarini.
Aidha ameipongeza TBS kwa kuendelea kushirikiana na ZBS ambayo kwasasa inaendelea kufanya vizuri tofauti na kipindi cha nyuma.
Kwa upande wake Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe kupitia ziara hiyo wanamatumaini yakuwa Kamati hiyo wataenda kusaidia kutoa elimu kwa wazalishaji kuhakikisha wanazalisha bidhaa kwa viwango ambavyo vimewekwa na Mashirika TBS na ZBS.
Amesema Wizara imefurahishwa kwa wenzao kuja kuwatembelea na kujifunza lakini zaidi kuimarisha ushirikiano katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu pande hizi mbili ndizo zinazounda Muungano uliopo.
“Tumepata mawazo namna ya kuendelea kuboresha utendaji wa Shirika letu la Viwango kwasababu pamoja na mambo mengine tunaamini kukaa pamoja na kushirikiana sisi kama taasisi kwa upande wa TBS na ZBS ili tufikie ushindani kwenye masoko ya kimataifa kwa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi na kuwalinda walaji wetu wanaotumia bidhaa zinazozalishwa kutoka nje ya nchi”. Amesema
Pamoja na hayo Naibu Waziri Kigahe amesisitizia TBS kuendelea kuwawezesha ZBS ambao wanahitaji kujengewa uwezo ili na wao waendelee kufanya kazi zao vizuri kama wanavyofanya TBS kwa upande wa bara.
Nae Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Zanzibar Mhe.Omar Shaaban amesema mafanikio ya Taasisi hizo yametokana na uongozi bora uliopo, hivyo ushirikiano huo utaenda kuendeleza mafanikio makubwa ambayo wananchi wanayahitaji kupitia Taasisi hizi mbili TBS na ZBS.