MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akikabidhi majiko banifu 114 yanayotumia nishati safi na Salama ya kupikia katika hafla iliyofanyika wilaya ya Bahi katika Vijiji vya Zanka na Kigwe yaliyotolewa na Jumuiya ya Wanawake wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,akizungumza wakati wa hafla ya Kukabidhi Mitungi ya Gesi na Majiko Banifu kwa Wananchi wa Vijiji vya Zanka na Kigwe Wilaya ya Bahi yaliyotolewa na Jumuiya ya Wanawake wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
MKURUGENZI wa Uendelezaji Masoko na Teknolojia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Advera Mwijage,akielezea lengo la kutoa Misaada hiyo ya Mitungi ya Gesi na Majiko Banifu kwa Wananchi wa Vijiji vya Zanka na Kigwe Wilaya ya Bahi yaliyotolewa na Jumuiya ya Wanawake wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
MKUU wa Wilaya ya Bahi,Godwin Gondwe,akizungumza wakati wa hafla ya Kukabidhi Mitungi ya Gesi na Majiko Banifu kwa Wananchi wa Vijiji vya Zanka na Kigwe Wilaya ya Bahi yaliyotolewa na Jumuiya ya Wanawake wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
SEHEMU ya Wananchi na Wanafunzi wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (hayupo pichani),akizungumza wakati wa hafla ya Kukabidhi Mitungi ya Gesi na Majiko Banifu kwa Wananchi wa Vijiji vya Zanka na Kigwe Wilaya ya Bahi yaliyotolewa na Jumuiya ya Wanawake wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,akimsikiliza Mkurugenzi wa Uendelezaji Masoko na Teknolojia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Advera Mwijage,wakati akielezea jinsi wananchi watakavyotumia Mitungi ya Gesi na Majiko Banifu katika Vijiji vya Zanka na Kigwe Wilaya ya Bahi yaliyotolewa na Jumuiya ya Wanawake wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akikabidhi majiko banifu 114 yanayotumia nishati safi na Salama ya kupikia katika hafla iliyofanyika Wilaya ya Bahi katika Vijiji vya Zanka na Kigwe yaliyotolewa na Jumuiya ya Wanawake wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Kukabidhi Mitungi ya Gesi na Majiko Banifu kwa Wananchi wa Vijiji vya Zanka na Kigwe Wilaya ya Bahi yaliyotolewa na Jumuiya ya Wanawake wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani..
Na.Alex Sonna-BAHI
KUELEKEA siku ya wanawake duniani Jumuiya ya wanawake wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamekabidhi misaada ya mitungi ya gesi na majiko banifu yanayotumia kuni na mkaa mchache ili kupunguza athari za uharibifu wa mazingira katika vijiji vya Zanka na Kigwe.
Msaada huo wameukabidhi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule katika vijiji vya Zanka na Kigwe wilayani Bahi.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Senyamule amewapongeza wanawake hao wa REA kwa kuonesha kuwajali wanawake wenzao pamoja na kutunza mazingira.
“Leo tupo na Rea tumeshuhudia namna bora walivyoamua kuadhimisha siku hii,jamani hongereni sana mmeamua kushiriki kwa upendo mkubwa sana,”amesema RC Senyamule
Amesema wanawake wanapata athari nyingi kwa kutumia kuni mojawapo ni magonjwa ya kiafya kwa maana ya macho na kifua hivyo kujikuta wakishindwa kuendelea na uzalishaji na badala yake kaunza kujitibu.
Aidha,Senyamule amempongeza Rais Samia kwa kuendeleza kuhamasisha utunzaji wa mazingira.
“Sisi Tanzania tunajivunia sana kwa kuwa na kiongozi Mkuu mwanamke imara jasiri mchapakazi Samia Suluhu Hassan ni mara yakwanza kwa Nchi yetu kupata kiongozi ambaye ni mwanamke
Amesema wanajivunia kazi kubwa ambayo anaifanya ikiwemo kuhakikisha wanawake wanazidi kupata fursa mbalimbali.
Katika hatua nyingine Senyamule amesema Serikali ya Mkoa inaweka mikakati ya kuhakikisha inaulinda msitu wa Chinene.
Amesema Serikali imejipanga kuwachukulia hatua kali wanaoharibu mazingira na inaandaa operation maalum kuuulinda msimu huo.
“Sisi hapa Zanka tunajua msitu wa Chinene umekuwa ukiharibiwa sana matumizi ya nishati mbadala yatasaidia sana utunzaji wa mazingira.Mkurugenzi Rea amesema inawezekana upungufu wa mvua unasababisha na ukataji wa miti hivyo majiko haya yatasaidia sana utunzaji wa mazingira,”amesema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uendelezaji Masoko na Teknolojia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Advera Mwijage, amesema wameamua kuwasaidia wakazi wa vijiji vya Zanka na Kigwe kutokana na umaskini uliopo katika maeneo hayo.
“REA tumekuja kuhamashisha jamii tunaenda kuwekeza nguvu katika nishati ya kupikia ni kama hizi mmeona majiko ambayo yanatumia mkaa kidogo unapika vyakula vingi.
“Tumekuja na mitungi ya gesi kilo sita,15 lengo kuwaonesha wananchi unaweza kupika kwa kutumia teknolojia mbalimbali.
“Nitoe shukrani kwa wanawake wote waliojichangisha kwa ajili ya kufanya hichi kitu kwa mtu yoyote mwenye uwezo sadaka sio lazima kanisani ni pamoja na namna hii,”amesema Mhandisi Advera
Amesema kina mama wengi wamekuwa wakijishughulisha na ujasirimali hivyo wanaamini watapa muda mwingi wa kufanya biashara kuliko awali walivyokuwa wakiutumia kutafuta kuni.
Aidha Mhandisi Advera amesema wanaendelea na mipango ya muda mrefu kusambaza gesi asilia inayotoka katika maeneo ya Lindi na Mtwara.
Amesema watasambaza nchi nzima lengo likuwa ni kuhakikisha mazingira yanakuwa salama.