Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akimkabidhi Naibu wake Bw.Geofrey Pinda kadi ya pongezi iliyosainiwa na viongozi wakuu wa Wizara mapema jana katika Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dodoma, kulia kwake ni Mhandisi Anthony Sanga Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi akifuatiwa na Bi.Lucy Kabyemela Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Viongozi wakuu wa Wizara ya Ardhi wakiwa katika picha ya pamoja, wa kwanza kushoto ni Naibu Wizara ya hiyo Geofrey Pinda akifuatiwa na Waziri Dkt. Angeline Mabula ambaye kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mhandisi Anthony Sanga akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu wake Bi. Lucy Kabyemela.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga muda mfupi baada ya kupolewa Wizarani hapo tayari kwa majukumu mapya ya kikazi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Bi. Lucy Kabyemela muda mfupi baada ya kupolewa Wizarani hapo tayari kwa majukumu mapya ya kikazi.
Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akimkaribisha Naibu wake Bw. Geofrey Pinda kwa mara ya kwanza ofisini kwake muda mfupi baada ya kupolewa Wizarani hapo tayari kwa majukumu mapya ya kikazi.
Na Anthony Ishengoma- DODOMA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Geofrey Pinda ameahidi kushirikiana na watendaji wakuu wa Wizara pamoja na maofisa wa sekta ya ardhi nchini ili kuhakikisha sekta hiyo hapa Nchini inasimamiwa vizuri na kutoa matokeo makubwa kwa wananchi.
Naibu Waziri Pinda amesema hayo leo tarehe 6, Machi 2023 alipowasili kwa mara ya kwanza tangu alipotelewa kuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo hivi karibuni na kukutana na Managementi ya Wizara kwa ajili kufahamiana lakini pia kupata fursa ya kujenga uelewa wa pamoja kuhusu Wizara ya Ardhi.
Kabla ya kukutana na Managementi ya Wizara awali Naibu Waziri Pinda alipokelewa kwa shangwe na watumishi wa Wizara yake mpya waliojitokeza kwa wingi kwa ajili ya mapokezi yake na wote walisikika wakiimba wimbo wa kuwa na imani kubwa nayeye ambaye pia aliwasilimia katika hali kubwa watumishi hao.
Kiongozi huyo mpya katika Wizara ya Ardhi alisema kuwa ni matarajio yake kuwa atapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa watendaji wa Wizara ili aweze kumsaidia Waziri wake lakini pia kukidhi matarajio ya wananchi hususani baada ya serikali kufanya mabadiliko ya uongozi katika sekta mbalimbali serikalini.
Akiongelea suala la wananchi kuchangia mapato ya serikali kupitia pango la ardhi Naibu Waziri Pinda alibainisha kuwa kwa sasa inawezekana kuna changamoto katika mfumo uliopo hivyo Wizara itahakikisha inafanya maboresho kujenga mfumo rafiki utakaowezesha wananchi kulipa kodi ya pango la ardhi bila usumbufu wowote.
Aidha Pinda aliongeza kuwa katika kukabiliana na changamoto iliyopo ya kimfumo juhudi zilizopo ni kushirikisha wananchi ili waweze kutambua umuhimu wa kulipa kodi ya ardhi lakini pia kuonesha umuhimu wa mchango wetu katika katika kukuza pato la taifa kwani ardhi ndiyo kila kitu.
Naibu Waziri huyo amesema kuwa atatumia fursa yake kujenga upendo miongoni mwa watumisha pamoja na kuwapa motisha na kutambua utaalamu wao ili watumishi wa sekta ya ardhi katika ngazi zote waweze kujenga umoja katika utekelezaji kazi kama hatua muhimu ya kuleta mageuzi kiutendaji katika sekta ya ardhi kote Nchini.