Meneja Masoko na Uhamasishaji wa mfuko wa Self Mirofinance Fund, Linda Mshana, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Dodoma na Singida kuhusu shughuli zinazofanywa na SELF MF katika kukuza uchumi kwa Wananchi.
Na Dotto Mwaibale, Dodoma
MFUKO wa SELF MICROFINANCE FUND uliopo
chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ambao una jukumu la kutoa huduma za kifedha
kwa wananchi wenye kipato cha chini umetoa mikopo ya Sh.bilioni 313 kwa
wanufaika 225,000.
Meneja Masoko na Uhamasishaji wa mfuko huo, Linda Mshana, akizungumza
wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Dodoma na Singida kuhusu
shughuli zinazofanywa na SELF MF katika kukuza uchumi kwa Wananchi alisema
mikopo hiyo imetolewa katika kipindi cha kuanzia 2000 hadi 2022.
Alisema mikopo hiyo yenye masharti nafuu imetolewa kwa wajasiriamali
wadogo, taasisi za fedha,benki za kijamii na Vyama vya Kuweka na Kukopa
(SACCOS) na kwamba mfuko ulianza na mtaji wa Sh.Bilioni 62 lakini kutokana na
marejesho mazuri kutoka kwa wakopaji ambayo ni takribani asilima 93 mtaji wa
mfuko umefikia Sh.bilioni 313 ambazo zimekopeshwa kwa wajasiriamali.
Mshana
alisema mikopo hiyo inayo lenga kuwapa watu fursa ya kufanya shughuli za
uzalishaji mali itasaidia kukidhi mahitaji ya kifedha kwa makundi mbalimbali ya
watu wakiwamo wakulima, wafugaji na wafanyabiashara.
“Moja
ya jukumu letukubwa ni kuwapa watu fursa
ya kufanya kazi kwa kutoa huduma ndogo za fedha kwa masharti nafuu na kuwa
jambo la msingi kwa wakopaji wanatakiwa kuwa waadilifu, wenye umoja, wabunifu
na wawajibikaji katika kujiletea maendeleo endelevu,” alisema Mshana.
Aziza
Nasibu ambaye ni mmoja wa wanufaika wa mfuko huo alisema anaushukuru Mfuko wa
Self Microfinance kwani umesaidia kuongeza mtaji wa biasharayake.
Aziza
ambaye anamili Kiwanda cha Cal Plastick mjini hapa ambacho kinachakata makopo
hususan ya maji,alisema mfuko huo ulimkopesha sh. Milioni 50 ambazo zilisaidia
kuinua kiwango cha biashara yake.
Mnufaika
mwingine wa mfuko huo Wema Sehaba ambaye anafanya bishara ya kuuza pembejeo za
kilimo alisema mfuko huo umemkopesha Sh.milioni 40 ambazo zimemsaidia kukuza
mtaji wa biashara yake.
Wema
alisema miezi miwili ijayo atakuwa amemaliza kurejesha marejesho ya mkopo huo
wa awali na kwamba anatarajia kukopa Sh.milioni 80 ambazo pamoja na mambo
mengine atafungua maduka ya pembejeo za kilimo nje ya mkoawa Dodoma.
Meneja wa Tawi la Dodoma, Aristid Tesha, amesema mikopo inayotolewa na
mfuko huo inakuwa na bima isipokuwa ile inayotolewa kwa kampuni na kwamba bima
inayotozwa kwa mteja ni asilimia 0.6 kwa mwaka na inamsaidia mteja anapopatwa
na majanga na kukwama kurejesha mkopo wake.
Tesha, alisema ofisi yao ya Dodoma ipo Makaru njia pada ya kwenda majumba
sita kushoto linaonekano bango kubwa na kulia kuna kituo cha bodaboda.
Muonekano wa ofisi ya mfuko huo iliyopo Dodoma eneo la Makuru njiapanda ya kwenda majumba Sita Barabara kuu ya kwenda Chuo Kikuu cha UDOM.