Afisa Rasilimali watu wa Kiwanda cha Bia cha TBL Tawi la Mwanza, Dora Nyambalya, akiwakabidhi taulo za kike walimu wa Shule ya Sekondari Mtoni, Rhoda Magesse (kushoto) na Jacqueline Joseph,zilizonunuliwa kutokana na michango ya wafanyakazi.

Walimu wa  Sekondari Mtoni Rhoda Magesse na Jacqueline Joseph (katikati) wakifurahi sambamba na Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha bia cha TBL tawi la Mwanza,wakati wakipokea taulo za kike  zenye thamani ya Shilingi 650,000, zilizotolewa na wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Shehena ya vita via hedhi iliyotolewa na wafanyakazi wa TBL Mwanza 

 …………………..

Katika mwendelezo wa kukabiliana na changamoto ya vifaa vya hedhi kwa wasichana wanaotoka kwenye  familia zenye mazingira magumu, wafanyakazi wa TBL wa kiwanda cha Mwanza wametoa msaada wa taulo za kike kwa shule ya sekondari ya Mtoni iliyopo mkoani humo.

Wafanyakazi wa kampuni hiyo katika viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam,Mbeya na Arusha nao tayari wameishatoa taulo hizo kupitia taasisi ya Her Africa kwa ajili ya wasichana wanaosoma shule mbalimbali ambao ni walengwa wa msaada huo.

Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo, Afisa Raslimali Watu wa kiwanda cha TBL cha Mwanza, Dorah Nyambalya, alisema kuwa msaada huo unatokana na michango ya wafanyakazi ambao wameguswa na tatizo la changamoto ya vifaa vya hedhi mashuleni. 
“Kupitia sera ya kampuni yetu yak kujenga Dunia Maridhawa wafanyakazi wa kampuni tunao wajibu wa kushiriki kukabiliana na changamoto mbalimbali katika mazingira yetu kama ambavyo safari hii tumeamua kusaidia wasichana mashuleni vifaa vya kuwastiri wakati wa vipindi vya hedhi ili waweze kusoma wakiwa katika mazingira rafiki”alisema Nyambalya.

Kwa upande wake Mwalimu,  Rhoda Magese,  kutoka shule ya sekondari ya Mtoni, iliyopo mjini Mwanza,alishukuru TBL  na wafanyakazi wake kwa jitihada za kusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali katika jamii.